Flandria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha zinazoonesha njia za njia za usafiri, Flandria
Bendera ya Flandria
Eneo la Flandria katika Ubelgiji

Flandria (Kiholanzi: Vlaanderen) ni jimbo la kaskazini kati ya majimbo matatu ya Ubelgiji. Lugha rasmi katika mikoa 5 ya jimbo ni Kiholanzi inayoitwa hapa Kiflaams ingawa ni lugha ileile. Idadi ya wakazi ni milioni 7. Serikali ya Flandria iko Brussels na mji mkubwa ya Flandria yenyewe ni Antwerpen.

Kihistoria Flandria ilikuwa kubwa zaidi ikajumlisha maeneo ya Ubelgiji, Ufaransa na Uholanzi wa leo. Utamaduni wake ni Kiholanzi lakini sehemu hii ilitawaliwa kwa muda mrefu na Hispania iliyowafukuza Waprotestant wote. Mwaka 1815 Flandria pamoja Ubelgiji wote uliunganishwa na Uholanzi lakini tofauti za kidini na kiutamaduni zilisababisha mapinduzi ya Ubelgiji ya 1830 yaliyoleta uhuru wa Ubelgiji kama taifa la pekee.

Siku hizi Flandria ni sehemu ya Ubelgiji inayostawi vema kiuchumi. Kuna harakati ya kisiasa inayodai Flandria kuwa nchi ya pekee.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ubelgiji bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Flandria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.