Nenda kwa yaliyomo

Fezolinetanti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fezolinetanti (Fezolinetant), inayouzwa kwa jina la chapa Veozah, ni dawa inayotumika kutibu hisia ya ghafla ya joto katika sehemu ya juu ya mwili hasa juu ya uso, shingo na kifua (hot flashes) kutokana na kukoma hedhi. Dawa hii hasa hutumiwa kwa dalili za wastani au kali.[1] Inachukuliwa kwa mdomo.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya tumbo, kuhara, matatizo ya kulala, maumivu ya mgongo, na matatizo ya ini.[1] Matumizi yake haipendekezwi kwa wale walio na matatizo makubwa ya figo au ini. [1] Ni kizuia cha vipokezi vya neurokinin-3 (NK 3).[1]

Fezolinetanti iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2023.[1] Nchini Marekani inagharimu takriban dola 560 za Marekani kwa mwezi kufikia mwaka wa 2023.[2] Mtengenezaji wake alituma maombi ya kuidhinishwa Ulaya mwaka wa 2022.[3]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Veozah- fezolinetant tablet, film coated". DailyMed. 19 Mei 2023. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Mei 2023. Iliwekwa mnamo 24 Mei 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Fezolinetant". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Machi 2024. Iliwekwa mnamo 13 Agosti 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Inc, Astellas Pharma. "European Medicines Agency Accepts Astellas' Marketing Authorization Application for Fezolinetant". www.prnewswire.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Oktoba 2022. Iliwekwa mnamo 13 Agosti 2023. {{cite web}}: |author= has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fezolinetanti kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.