Feng Bin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Feng Bin (Alizaliwa Aprili 3,1994) ni mwanariadha kutoka nchini china hushiriki mchezo wa kurusha kisahani. Aliiwakilisha nchi yake katika mashindano ya Olimpiki jijini Rio mwaka 2016, akimaliza nafasi ya nane katika fainali. Rekodi yake bora ni mita 65.14 (213 ft 8+1/2 in),[1] aliyoiweka mwaka 2016[2]. Mnamo 2016 alikuwa mshindi wa michuano ya Chinese Athletics Championships[3].

Alianza mchezo wa kurusha kisahani akiwa katika umri wa ujana, na alishindana katika michuano ya World Youth Athletics ya mwaka 2011[4], nakushikilia nafasi ya 4. Feng aliendelea kwenye ngazi za juu na kushinda medali ya dhahabu mwaka 2015, kwenye michezo ya kijeshi duniani kwa rekodi yake ya mita[5] 62.07. Katika mashindano ya olimpiki msimu wa joto 2016 alikuwa mshiriki mmojawapo kati ya watatu warusha visahani  kufika fainali akiwa pamoja na mshindi wa medali Su Xinyue na Chen Yang[6].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. www.rio2016.com
  2. "Wlodarczyk throws world-leading 79.48m in Halle | REPORT | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-09-25. 
  3. www.all-athletics.com
  4. "Bin FENG | Profile | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-09-25. 
  5. "Mixed fortunes for world champions at World Military Games | REPORT | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-09-25. 
  6. "China.com - Your guide on traveling and living in China". english.china.com. Iliwekwa mnamo 2021-09-25. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Feng Bin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.