Fatma Abdulhabib Fereji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fatma Abdulhabib Fereji (amezaliwa 26 Julai 1961) ni mbunge katika baraza la wawakilishi la Zanzibar, Tanzania.[1] kupitia chama cha Civic United Front (CUF).

Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Darajani kuanzia mwaka 1967 hadi 1973 na elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Hamamni (1974-1976) na kuhamia katika katika Chuo cha Lumumba kwa ajili ya masomo ya sekondari ngazi ya awali na mwisho kuanzia (1977-1980) na baadae alipata shahada ya kwanza ya Ualimu wa sanaa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1983-1986) na shahada ya uzamili ya ukutubi katika chuo kikuu cha Wales, Ufalme wa Muungano (1989-1991)[2]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. [Mengi kuhusu Fatma Abdulhabib Fereji. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-09-08. Iliwekwa mnamo 2010-11-13. Mengi kuhusu Fatma Abdulhabib Fereji]
  2. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-01-26. Iliwekwa mnamo 2020-01-26.