Fatimé Dordji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fatimé Dordji, pia anayejulikana kama Fatimé N'Dordji (14 Julai 1949 - 30 Novemba 2016) alikuwa mwanabiashara na mwandishi wa habari kutoka Chad. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuajiriwa kama mtangazaji wa redio katika nchi hiyo.


Maelezo binafsi[hariri | hariri chanzo]

Dordji alizaliwa tarehe 14 Julai 1949 huko Ati, Chad. Alikulia katika mji wa Sarh na mama yake, ambaye alikuwa Mwarabu, na baba wa kambo ambaye alifanya kazi kama askari. Akiwa na umri wa miaka kumi na nne, alihamia N'Djamena, ambapo alipata kazi kama mtangazaji wa redio kutokana na ujuzi wake wa Kifaransa na Kiarabu. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuajiriwa katika jukumu kama hilo. Kufikia mwaka 1965 alikuwa mtu mashuhuri katika redio ya Radiodiffusion Tchadienne. Mwaka huo huo aliolewa na polisi, na baadaye mwanasiasa, anayeitwa Senoussi Khater na ambaye walizaa watoto saba pamoja.[1]

Mwaka 1973, Dordji alianza kutazamwa kama adui wa serikali, baada ya kumtaja moja wa binti zake kwa jina la mwanasiasa Kalthouma Nguembang, ambaye Rais François Tombalbaye alikuwa amemtuhumu kujaribu kutumia uchawi dhidi yake. Aliwekwa kizuizini na baadaye akazuiliwa na polisi kwa zaidi ya miezi ishirini na moja.[1] ingawa kamwe hakufunguliwa mashtaka rasmi ya shughuli za ualifu.[2]

Mwaka 1975 Félix Malloum alimpindua Tombalbaye, na mume wa Dordji aliteuliwa kuwa Balozi nchini Libya katika serikali mpya. Kuanzia mwaka 1978 hadi 1981 familia iliishi Ubelgiji. Hata hivyo, wakati huu yeye na mume wake walitalakiana: Mume wake alirudi Chad kuwa Waziri wa Elimu katika serikali mpya, yeye alikwenda Libya.[1]

Katika miaka ya 1990, chini ya serikali mpya ya Idriss Déby, Dordji alirudi Chad akifanya kazi kwanza kama mtangazaji wa redio, kisha baadaye kama mfanyabiashara.[1] Alifariki tarehe 30 Novemba 2016.[3]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 Rich, Jeremy (2011-01-01), "Dordji, Fatimé", Dictionary of African Biography (kwa Kiingereza) (Oxford University Press), ISBN 978-0-19-538207-5, doi:10.1093/acref/9780195382075.001.0001/acref-9780195382075-e-0576?rskey=1qdelt&result=576, iliwekwa mnamo 2022-09-06 
  2. colaborador. "Fatimé Dordji (1949)". Biografias de Mulheres Africanas (kwa pt-BR). Iliwekwa mnamo 2022-09-07. 
  3. Genealogie, Coret. "Death Fatime N'Dordji on November 30, 2016 in Tours, Indre-et-Loire, Centre-Val de Loire (France)". Open Archives (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-09-07. 
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fatimé Dordji kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.