Fatema Mernissi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mernissi akipokea Tuzo ya Erasmus, 2004
Mernissi akipokea Tuzo ya Erasmus, 2004

Fatema Mernissi (Kiarabu: فاطمة مرنيسي , kiromania: Fāṭima Marnīsī; 27 Septemba 1940 - 30 Novemba 2015) alikuwa mwandishi na mwanasosholojia wa Moroko.

Wasifu.[hariri | hariri chanzo]

Fatema Mernissi alizaliwa tarehe 27 Septemba 1940 huko Fez, Moroko. Alilelewa katika nyumba ya bibi yake pamoja na jamaa na watumishi mbalimbali wa kike.[1]Alipata elimu yake ya msingi katika shule iliyoanzishwa na wanaharakati wa kitaifa, na elimu ya sekondari katika shule ya wasichana iliyofadhiliwa na jeshi la ulinzi wa Ufaransa.[2]

Marejeo.[hariri | hariri chanzo]

  1. Gayatri Devi (2015-12-18). Fatima Mernissi obituary (en). the Guardian. Iliwekwa mnamo 2022-03-01.
  2. Mernissi, Fatima (1987). Beyond the veil : male-female dynamics in modern Muslim society, Internet Archive, Bloomington : Indiana University Press. ISBN 978-0-253-31162-7.