Faeqa bint Saeed Al Saleh

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Faeqa bint Saeed Al Saleh ni mwanasiasa na waziri wa afya wa Bahrain.[1][2]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alihitimu kutoka chuo cha Uingereza na akatunukiwa shahada ya uzamivu wa masomo ya upangiliaji wa taarifa (Library and Information Studies). Alihudumu kama msaidizi wa katibu mkuu wa maswala ya kijamii katika mataifa ya Kiarabu. Alihudumu pia kama waziri wa maendeleo ya jamii kutoka Disemba 2014 hadi alipochaguliwa kama waziri wa afya Oktoba mwaka 2015. Jarida la Forbes Mashariki ya kati lilimtaja kama mtu wa tisa kwa ushawishi kwenye orodha ya wanawake waliopo serikalini.Alikuwa ni mwanamke pekee baraza la mawaziri la Bahrain. Disemba 2015 alisheherekea siku ya wanawake nchini Bahraini katika maswala ya kiafya, na aliahidi kusaidia makada wa kike na washiriki wao katika wizara. Chini ya uongozi wake wizara ya afya na wizara ya mambo ya nje ziliungana na katika kuanzisha chuo cha mfalme Hamadi nchini Pakistani. Chini ya wakati alizindua hoteli yenye kliniki nchini Bahrain ya 'Four Seasons'.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Health Minister briefed on Galali citizens' needs", Bahrain News Agency. Retrieved on 7 November 2017. 
  2. "Health Minister visits Hoora, Qudaibiya", Bahrain News Agency. Retrieved on 7 November 2017.