Elián González
Elián González Brotons (alizaliwa Desemba 6, 1993) ni mhandisi wa kiwanda na mwanasiasa kutoka nchini Cuba. Akiwa kijana wa miaka mitano, alijikuta katikati ya mgogoro mkubwa wa kidiplomasia kati ya Marekani na Cuba mwishoni mwa mwaka 1999 na mapema 2000. Ulimwengu ulimfahamu akiwa na umri wa miaka 5. Hilo lilitokana kwa kunusurika kwake katika ajali ya boti iliyochukua uhai wa mama yake wahamiaji wengine waliokuwa wakijaribu kuvuka Bahari ya Atlantiki kutokea Cuba kwenda Marekani.
Mnamo Novemba 25, 1999, Elian alikutwa akielea juu ya mgongo wa tairi la gari karibu na pwani ya Florida. Ni baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama. Uokozi ulipotimu, akawekwa chini ya uangalizi wa jamaa zake waliokuwa wakiishi Miami, Marekani. Tukio hili liliibua mvutano mkubwa kati ya familia ya Elian ya nchini Marekani, ilitaka abaki nchini humo. Ilhali baba yake, Juan Miguel Gonzalez, aliyekuwa upande wa Cuba, alidai kijana wake arudishwe Cuba.
Serikali ya Marekani chini ya uongozi wa Rais Bill Clinton ilikabiliwa na shinikizo kubwa kutoka pande zote mbili. Familia ya Elian huko Miami iliungwaji mkono kutoka kwa jamii ya wahamiaji wa Cuba waliokuwa na hasira kali dhidi ya utawala wa Fidel Castro. Pamoja na yote, baada ya miezi kadhaa ya mivutano ya hapa na pale ya kisheria na kisiasa, Mahakama ya Marekani iliamua kwamba Elian arudishwe kwa baba yake huko Cuba. Uamuzi huu ulitekelezwa kwa nguvu mnamo Aprili 22, 2000. Baada ya maamuzi ya mahakamani, akina FBI waliingia kwa nguvu katika makazi ya ndugu wa Elian huko mjini Miami na kumchukua kwa nguvu kwa minajili ya kurudishwa kwa baba yake.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- History.com - Elian Gonzalez
- CNN - Elian Gonzalez: What happened?
- Chomsky, Aviva. *The Cuba Reader: History, Culture, Politics*. Duke University Press, 2019.
- Menéndez, Alberto. "The Elian Gonzalez Case: Child, Family, and Politics." *Journal of American Studies* 35, no. 2 (2001): 157–174.
- De La Torre, Miguel A. *La Lucha for Cuba: Religion and Politics on the Streets of Miami*. University of California Press, 2003.
- The New York Times - Father and Son Arrive Home in Cuba
- The Guardian - Elian Gonzalez returns to Cuba
- The Washington Post - The Elian Gonzalez Case: Timeline
- USA Today - Elian Gonzalez, 15 years later
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Elián González kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |