Nenda kwa yaliyomo

Eilish Flanagan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Eilish Flanagan (alizaliwa 2 Mei 1997) ni mwanariadha wa mbio ndefu wa Irelandi.[1] Kutoka Gortin kwenye jimbo la Tyrone, Flanagan alisoma chuo cha Sacred Heart, Omagh kabla ya kupata ufadhili katika chuo cha Adam State Kolarado.[2] Wakati akiwa katika chuo cha Adams State aliweka rekodi mpya ya NCAA Division II katika mita 1500, na kushinda michuano ya riadha za nje za 2021 NCAA Division II kwenye mita 3000 mbio za mwinuko, pia alimaliza mbio za mita 5000 mwaka 2021 na mita 6000 kwenye Cross country race ya 2019. Alikimbia kwa ajili ya Omagh Harriers na Carmen Runners Athletics Club.[3] Pacha wake Roisin ni mwanaridha wa mbio Ndefu na mnufaika wa ufadhili wa chuo cha Adams State na anashikilia rekodi nchini Irelandi yam bio za mita 5000. Mapacha hao walikuwa katika timu ya Irelandi iliyoshinda medali ya fedha kwa walio chini ya umri wa miaka 23 katika michuano ya European Cross Country jijini Lisbon.[4]

  1. "Eilish FLANAGAN | Profile | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-02.
  2. "Eilish Flanagan - Women's Cross Country". Adams State University Athletics (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-10-02.
  3. "Athlete Profile". www.thepowerof10.info. Iliwekwa mnamo 2021-10-02.
  4. "Flanagan moves into Tokyo contention", BBC Sport (kwa Kiingereza (Uingereza)), iliwekwa mnamo 2021-10-02