Nenda kwa yaliyomo

Double Double

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Double Double"
"Double Double" kava
Wimbo wa Nyandu Tozzy akiwa na Young Dee na Chin Bees
Umetolewa 2017
Umerekodiwa 2017
Aina ya wimbo Hip hop
Urefu 3:46
Mtunzi Nyandu Tozzy

"Double Double" ni jina la wimbo kutoka kwa msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania, Nyandu Tozzy. Ndani yake ameshirikishwa Chin Bees na Young Dee. Chin Bees amesimama kwenye kiitikio, wakati Young Dee ametambaa katika ubeti wa pili. Mashairi ya Nyandu hasa yanaelezea hasa wasanii wachanga wanaongia katika muziki na kupata mafanikio ya awali punde wanaanza dharau na kuona hata waliotangulia hawana maana. Nyandu anasema hata yeye mwenyewe haonekani sana kibwege na mara nyingi anakuwa kwenye gari lenye kioo cha kiza, ila amekuwa anajichanganya katika shughuli mbalimbali bila kubagua wengine. Mwishoni anawatakia heri marafiki zake walioko jela. Ubeti wa pili anaanza Young Dee anayejisifu kwa kutoringa, lakini ana akili nyingi. Isitoshe siku hizi muziki ni kazi, hawezi kufanya kazi bila malipo. Anawaponda wale ambao wanamuona hana akili. Mikwara ya mchana David, usiku paka.[1]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Double Double New Video: Nyandu Tozzy ft Chin Bees & Young Dee – Double Double kwenye Bongo5.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]