Domain name

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Domain name ni jina ambalo ni kama kitambulisho na linafafanua ulimwengu wa utawala, uhuru mamlaka wa wavuti fulani katika mitandao.

Jina la domain hutengenezwa na katiba na utaratibu wa DNS. Jina lolote lililoandikishwa ndani ya DNS ni domain name.

Kwa ujumla, domain name husimamia anwani ya mitandao (ip), kama vile tarakilishi ya binafsi ambayo hutumika katika upatikanaji wa intaneti.

Kufikia mwaka 2017, domain name milioni 330.6 ziliandikishwa.

Mapendekezo ya domain name[hariri | hariri chanzo]

Domain name huwa na jina la biashara au shirika unalofanya kazi nalo ambalo ungetaka liwe na wavuti. Kwa mfano, jina kama 'Kiswahilikitukuzwe.org' linaashiria kuwa utakuwa ukijadili maswala ya kiswahili na hilo ni shirika kwa sababu ya jinsi domain yenyewe inaishia kwa .org.

Domain name za kibiashara huishia kwa '.com'. Huenda pia domain ikawa inaashiria mahala hilo shirika au biashara ipo kwa mfano .or.tz kuonyesha kuwa ii katika nchi ya Tanzania.