Nenda kwa yaliyomo

Djoumbé Fatima

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Djoumbé Fatima
Malkia
Tarehe ya kuzaliwa 1837
Tarehe ya kifo 1837


Djoumbé Fatima (pia anayejulikana kama Djoumbé Soudi au Malkia Jumbe-Souli, 1837 - 1878) alikuwa Sultani wa Mohéli huko Komori kuanzia mwaka 1842 hadi 1865, tena kuanzia mwaka 1874 hadi kifo chake mwaka 1878.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Jumbe-Souli alirithi kiti cha enzi cha kisiwa cha Moheli (Mwali) baada ya kifo cha baba yake, Mfalme Ramanateka, anayejulikana pia kama Sultan Abderahmane. Ramanateka alikuwa mwana wa kifalme wa Malagasy ambaye alikimbia kutoka Madagascar baada ya kifo cha Mfalme Radama I.[1] Pia alikuwa binamu wa Mfalme Radama II. Alikuwa na dada, Jumbe-Salama, ambaye alifariki akiwa mdogo.[2]

Mama yake alikuwa Mmerina wa Madagascar. Baba yake, Jenerali Ramanataka, alikuwa ndugu mkwe wa Radama I, Mfalme wa Madagascar. Aliaga dunia mwaka 1842 na Djoumbé akapanda kwenye kiti cha enzi. Mama yake, Ravao, alitawala kama msimamizi kwa muda na baadaye aliolewa na mshauri wa zamani wa mumewe, Tsivandini, mwaka 1843. Aliyegeuka kuwa mwalimu wa Djoumbé na kuanza kutengeneza mipango kwa ajili ya ndoa yake na sultani wa Zanzibar.[3] ISBN 978-2-7475-6953-8

Djoumbé Fatima
Born: 1837 Died: 1878
Regnal titles
Alitanguliwa na
Ramanetaka
Mohamed bin Saidi Hamadi Makadara
Queen (Sultan) of Mohéli (Mwali)
1842–1865
1874–1878
Akafuatiwa na
Mohamed bin Saidi Hamadi Makadara
Abderremane bin Saidi Hamadi Makadara
  1. "Five African queens you did not know existed - Page 3 of 6". Face2Face Africa (kwa Kiingereza). 2018-09-01. Iliwekwa mnamo 2019-12-04.
  2. CHARNAY, DÉSIRÉ (1862). MADAGASCAR VOL D'OISEAU. uk. 67.
  3. Sheldon, Kathleen (2005). "Djoumbe Fatima (1837–1878)". Historical Dictionary of Women in Sub-Saharan Africa. Lanham (Maryland): Scarecrow Press. uk. 63. ISBN 978-0-8108-5331-7.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Djoumbé Fatima kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.