Devin Booker

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Booker katika Mchezo wa Nyota Wote wa NBA 2022
Booker katika Mchezo wa Nyota Wote wa NBA 2022

Devin Armani Booker (alizaliwa 30 Oktoba 1996) ni mchezaji wa kulipwa wa mpira wa kikapu kutoka Marekani anayechezea Phoenix Suns ya ligi kuu ya mpira wa kikapu Marekani.

Ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu Melvin Booker[1]. Baada ya kuchezea mpira wa chuo kwa msimu mmoja na Kentucky Wildcats[2][3], Booker alichaguliwa kuchezea Phoenix Suns kwenye awamu ya kwanza ya mwaka 2015 kwa chaguo la 13. Mwaka 2017 tarehe 24 Machi aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kufunga point 60 kwa mchezo na kumaliza na pointi 70 dhidi ya timu ya Boston Celtics[4]. Machi 2019 akiwa na miaka 22, Booker alikuwa mchezaji mdogo kwenye historia ya shirikisho la mpira wa kikapu marekani kuwa na pointi 50 kwa michezo mfululizo. Booker alipokea tuzo kwa alizochaguliwa za NBA All-Star mwaka 2020 na 2021 kama mchezaji wa mbadala.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]