Deepika Narayan Bhardwaj

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Deepika Narayan Bhardwaj (alizaliwa 4 Desemba 1986) ni mwandishi wa habari raia wa India, mtengeneza filamu za makala na mwanaharakati wa haki za wanaume.[1][2] Bhardwaj alijizolea umaarufu baada ya kutengeneza makala ya—Mashahidi wa ndoa, ambayo inahusu unyanyasaji wa kijinai, chini ya kifungu namba 498A (Sheria ya kupinga mahari) wa bi harusi na familia zao.[3][1][4] Pia alifichua njama za wanaodaiwa kuathiriwa katika video yenye utata iliyosambaa ya wadada wa Rohtak kwa kuwahoji mashahidi na kukusanya ushahidi.[5]

Elimu na kazi[hariri | hariri chanzo]

Deepika Narayan Bhardwaj alihitimu shahada ya kwanza ya tekinolojia (B.Tech) kutoka taasisi ya tekinolojia ya ya nguo na sayansi (Technological Institute of Textile & Sciences (TITS)) mwaka 2006. Pia alihitimu stashahada ya uzamili (post-graduate Diploma) ya uandishi wa habari wa runinga (television journalism) kutoka taasisi ya Indian Institute of Journalism & New Media mwaka 2009.[6]

Pia alifanya kazi kama mhandisi wa programu (Software Engineer) katika taasisi ya Infosys kati ya 2006 to 2008[6] kabla hajaacha kazi na kuendelea na utengenezaji wa filamu.[7] Makala yake ya kwanza katika kazi ya filamu iitwayo Gramin Dak Sevak ilichukua tuzo ya mshindi wa filamu ya mwanafunzi katika mashindano ya Jeevika: Asia Livelihood Documentary Festival mwaka 2009.[8] Pia alifanya kama mhariri mshauri katika taasisi ya Exchange4Media tangu Novemba 2010.[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Deepika Narayan Bhardwaj kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.