Davinson Sanchez

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Davinson Sanchez

Dávinson Sánchez Mina (alizaliwa 12 Juni 1996) ni mchezaji wa soka wa Colombia ambaye anacheza katika klabu ya ligi kuu ya Uingereza iitwayo Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Colombia.

Tottenham Hotspur[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 18 Agosti 2017, klabu ya Ligi Kuu ya Tottenham Hotspur ilitangaza kwamba walikubaliana na Davinson Sánchez kusaini mkataba wa miaka sita chini ya kibali cha kazi, kwa ada ya uhamisho iliyofikia £ milioni 42.

Mnamo tarehe 15 Mei 2018, Sánchez alisaini mkataba mpya na Tottenham, akiweka mkataba hadi mwaka 2024.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Davinson Sanchez kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.