Nenda kwa yaliyomo

Daniel Cardoso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Daniel Antonio Cardoso (amezaliwa 6 Oktoba 1989) ni mchezaji wa soka wa Afrika Kusini anayeshiriki kama beki kwa klabu ya Sekhukhune United katika ''Premier Soccer League''.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Cardoso alizaliwa huko Mji wa ''Johannesburg''. Baba yake alikulia nchi ya Ureno, wakati mama yake ni mzaliwa wa Afrika Kusini.[1] Cardoso alitamani kuwa daktari wa wanyama, lakini alisitisha masomo yake mwaka 2003 ili kuanza kazi yake ya soka. Ingawa anapata R100,000 kwa mwezi, bado anashauri watu wakumbatie elimu.[2]

Maisha ya klabu

[hariri | hariri chanzo]

Cardoso aliteuliwa kuwa nahodha wa timu ya akiba mwaka 2014. Mwezi Julai 2014, Cardoso alipata jeraha la Mguu ambalo lilimweka nje kwa miezi mitano.[3] Cardoso alihamia Kaizer Chiefs tarehe 31 Mei 2015. Baada ya kutumia miaka 7 na Chiefs, Cardoso aliondoka tarehe 1 Juni 2022 na kuwa mchezaji huru.[4]

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Daniel Cardoso kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Sorry! website unavailable". diskifans.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-06-30. Iliwekwa mnamo 2023-06-10.
  2. "Know your Stars: Daniel Cardoso – Freestatestars". freestatestars.co.za. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-06-10. Iliwekwa mnamo 2023-06-10.
  3. "FSS Defender, Daniel Cardoso, Ruled Out Until August". South African soccer news. 8 Julai 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-07-04. Iliwekwa mnamo 2023-06-10.
  4. "Daniel Cardoso Has Completed His Move To Kaizer Chiefs". South African soccer news. 31 Mei 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-07-04. Iliwekwa mnamo 2023-06-10.