Dadji Rahamata Ahmat Mahamat
Dadji Rahamata Ahmat Mahamat ni mwanaharakati wa haki za wanawake wa Chad. Yeye ni meneja wa ofisi ya CAMOJET, Collectif des Associations et Mouvements de Jeunes du Tchad (Mkusanyiko wa Vuguvugu na Mashirika ya Vijana nchini Chad).
Maisha ya zamani
[hariri | hariri chanzo]Yeye ni binti wa Ahmat Dadji, Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Kampuni ya Chadian Industrial Sugar Company (SONASUT) na kiongozi wa watu wa Hadjeraï. [1]
Hajamwona baba yake tangu akiwa na umri wa miaka miwili. [2] [3] Tarehe 28 Mei 1987 baba yake na kaka zake wawili wakubwa wenye umri wa miaka 20 na 17 walikamatwa na watu wanaodaiwa kutumwa na Rais wa Chad Hissène Habré.
Tangu wakati huo, yeye na familia yake wamefanya kampeni ya kujua nini kilimpata baba yake na hii ndio sababu iliyo mvuta kwenye maswala ya uanaharakati kwa ujumla zaidi. [4]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Amefanya kazi kwenye mashirika na vyama mbalimbali nchini Chad, na alijiunga na CAMOJET mwaka wa 2010. [5]
Yeye ni conseillère du bureau (meneja wa ofisi) kwa Collectif des Associations et Mouvements de Jeunes du Tchad (Mkusanyiko wa Vuguvugu na Vyama vya Vijana nchini Chad) CAMOJET, "chama cha vijana kinachofanya kazi kwa ajili ya haki za binadamu" kilichoko mji mkuu wa nchi hiyo. mjini N'Djamena . [6] [7][8]
Tarehe 6 Februari 2015 Dadji alikamatwa lakini aliachiliwa baadaye siku hiyo kwa masharti kwamba asizungumze na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwake. [9] [10] Alizungumza mara moja na akakamatwa tena na kuachiliwa pamoja na waandamanaji wengine 22 bila kufunguliwa mashtaka tarehe 8 Februari na kuamuru kutozungumza tena na vyombo vya habari isipokuwa alitaka "kuharibu maisha yake". [6]
Dadji amesema, "Nimenyanyaswa kutishwa na kutishiwa lakini nitasimama kidete." [11]
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Dadji anaishi katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena. [12]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Dadji Rahamata Ahmat Mahamat: The courage to demand justice". www.amnesty.org. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Dadji Rahamata Ahmat Mahamat: The courage to demand justice". www.amnesty.org. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)"Dadji Rahamata Ahmat Mahamat: The courage to demand justice". www.amnesty.org - ↑ "May – 2017 – ILCAT - Blogs". topics.gcil-km.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Novemba 2017. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Dadji Rahamata Ahmat Mahamat: The courage to demand justice". www.amnesty.org. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)"Dadji Rahamata Ahmat Mahamat: The courage to demand justice". www.amnesty.org - ↑ "Dadji Rahamata Ahmat Mahamat: The courage to demand justice". www.amnesty.org. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)"Dadji Rahamata Ahmat Mahamat: The courage to demand justice". www.amnesty.org - ↑ 6.0 6.1 "BETWEEN RECESSION AND REPRESSION: THE RISING COST OF DISSENT IN CHAD", September 2017. Retrieved on 8 November 2017. Archived from the original on 2021-05-09.
- ↑ Mak. "Tchad: voici la liste des militants arrêtés par la police - Makaila, plume combattante et indépendante". makaila.fr. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-02-18. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Collectif des Associations et Mouvements de Jeunes du Tchad (CAMOJET)". peaceinsight.org. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "BETWEEN RECESSION AND REPRESSION: THE RISING COST OF DISSENT IN CHAD", September 2017. Retrieved on 8 November 2017. Archived from the original on 2021-05-09. "BETWEEN RECESSION AND REPRESSION: THE RISING COST OF DISSENT IN CHAD" Ilihifadhiwa 9 Mei 2021 kwenye Wayback Machine.. Amnesty.org. September 2017.
- ↑ Mak. "Tchad: voici la liste des militants arrêtés par la police - Makaila, plume combattante et indépendante". makaila.fr. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-02-18. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)Mak. "Tchad: voici la liste des militants arrêtés par la police - Makaila, plume combattante et indépendante" Ilihifadhiwa 18 Februari 2022 kwenye Wayback Machine.. makaila.fr - ↑ "Dadji Rahamata Ahmat Mahamat: The courage to demand justice". www.amnesty.org. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)"Dadji Rahamata Ahmat Mahamat: The courage to demand justice". www.amnesty.org. - ↑ "Collectif des Associations et Mouvements de Jeunes du Tchad (CAMOJET)". peaceinsight.org. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)"Collectif des Associations et Mouvements de Jeunes du Tchad (CAMOJET)". peaceinsight.org