Claudine André

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Claudine André ni mwanaharakati wa uhifadhi wa maliasili wa Ubelgiji. Alizaliwa huko La Hestre,tarehe 6 Novemba 1946. Alianzisha hifadhi inayoitwa Lola ya bonobo mnamo mwaka 1994, ambayo ni hifadhi maalumu kwa ajili ya jamii ya nyani wanaojulikana kama bonobo huko kusini mwa Kinshasa, Mont Ngafula, katika Bonde la Lukaya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo . [1]

Madhumuni ya hifadhi hiyo maalumu ni kukusanya bonobo wachanga, wengi wao wakiwa yatima kutokana na vitendo vya wawindaji haramu, na hatimaye kuwarudisha katika hifadhi ya msitu. Katika mwaka huo huo, Claudine André alianzisha kikundi cha Marafiki wa Wanyama nchini Kongo, ambako bado ni raisi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. The story of Lola ya Bonobo. Lola ya Bonobo. Jalada kutoka ya awali juu ya 5 June 2008. Iliwekwa mnamo 12 March 2011.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Claudine André kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.