Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah (KNUST), kinachojulikana kama UST, Tech au Kwame Tech, ni chuo kikuu cha umma kilichoko Kumasi, mkoa wa Ashanti, Ghana. Chuo kikuu hiki kinaangazia hususani sayansi na teknolojia.[1] Ni chuo kikuu cha pili cha umma kuanzishwa, vile vile ni chuo kikuu kikubwa zaidi katika Mkoa wa Ashanti nchini Ghana.[2]
KNUST iilikuwa katika mipango ya Agyeman Prempeh I, mtawala wa Ufalme wa Ashanti, kuanzisha chuo kikuu huko Kumasi kama sehemu ya harakati zake kuelekea kuufanya ufalme wake wa Ashanti kuwa wa kisasa.[3] Mpango huu haukutimia kamwe kutokana na mgongano kati ya upanuzi wa himaya ya Uingereza na hamu ya Mfalme Prempeh wa Kwanza kuhifadhi uhuru wa ufalme wake wa Ashanti.[4]Hata hivyo, kaka yake mdogo na mrithi wake, Mfalme Asantehene Agyeman Prempeh II, alipotawadhwa mwaka wa 1935, aliendelea na maono haya. [5]Matukio mbalimbali huko pwani ya dhahabu(Ghana) katika kipindi cha miaka ya 1940 yalitekelezwa chini ya uongozi wake. Kwanza, kulikuwa na uanzilishi wa Chuo Kikuu cha Gold Coast.[6] Pili, kulikuwa na ghasia za 1948 Accra na matokeo yake ripoti ya Tume ya Watson, ambayo ilipendekeza kwamba chuo kikuu cha sayansi kianzishwe Kumasi. Kwa hivyo, katika 1949, ndoto ya akina Prempeh ilitimia wakati ujenzi ulianza juu ya kile ambacho kingeitwa Chuo cha Teknolojia cha Kumasi.[7]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "The Campus | Kwame Nkrumah University of Science and Technology". www.knust.edu.gh. Iliwekwa mnamo 2024-07-13.
- ↑ Agyekum, Kofi; Simons, Barbara; Botchway, Seth Yeboah (2018-12-30). "Factors influencing the performance of safety programmes in the Ghanaian construction industry". Acta Structilia (kwa Kiingereza). 25 (2): 39–68. doi:10.18820/24150487/as25i2.2. ISSN 2415-0487.
- ↑ "Kwame Nkrumah University of Science and Technology", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-06-25, iliwekwa mnamo 2024-07-13
- ↑ "Kwame Nkrumah University of Science and Technology", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-06-25, iliwekwa mnamo 2024-07-13
- ↑ "Kwame Nkrumah University of Science and Technology", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-06-25, iliwekwa mnamo 2024-07-13
- ↑ "August 11, 1948: The University College of the Gold Coast is established by Ordinance". Edward A. Ulzen Memorial Foundation (kwa American English). 2017-08-11. Iliwekwa mnamo 2024-07-13.
- ↑ "January 22, 1952: Kumasi College of Technology is established". Edward A. Ulzen Memorial Foundation (kwa American English). 2018-01-23. Iliwekwa mnamo 2024-07-13.