Chuo Kikuu cha Abuja
Chuo Kikuu cha Abuja kilianzishwa tarehe 1 Januari, mwaka 1988 (chini ya agizo la NO. 110 la mwaka 1992 kama lilivyorekebishwa) kama chuo cha sura mbili chenye mamlaka ya kuendesha masomo chuoni na mpango wa elimu ya masafa ya mbali. Ndicho Chuo Kikuu cha kwanza cha Nigeria kuwa na uwezo wa aina hiyo, kwa hivyo chuo kimejitolea na kinajaribu kuhakikisha ufanisi wa elimu na wakati huohuo kikidumisha nafasi sawa za wananchi kupata elimu na kwa njia kinawatayarisha wanafunzi kwa majukumu yao muhimu katika jamii.
Wito wa Chuo hicho ni For Unity and Scholarship na chini usimamizi wa Naibu wa chuo wa sasa Prof Vicekansler Nuhu Yaqub anasema hali hii itatoa elimu ya ubunifu na tendeti inayozingatia huduma kwa binadamu, kwa hivyo katika kufikia malengo muhimu, kozi za chuo zinalenga kuwapa wanafunzi na wahadhiri mafunzo ambayo ni msingi katika kuwawezesha kuwa wabunifu na wenye kuibua mawazo mapya katika kutekeleza majukumu yao katika vipengele mbalimbali vya mahitaji ya binadamu ambavyowatajihusisha navyo.
Kwa sasa Chuo Kikuu cha Abuja kinatoa shahada za kawaida, Stashahada na Kozi za baada ya Uzamili na Uzamifu na kutokana na kuwa katika eneo la Utawala wa Shirikisho chuo hicho kina Kituo cha Masomo ya Mbali ambacho kinatoa nafasi za elimu ya vyuo vikuu kwa wale ambao kwa sababu moja au nyingine, hawawezi kupata elimu kama hiyo kupitia kwa elimu ya mfumo wa kawaida na pia wale ambao wangependa kupata maarifa mapya na ujuzi maalum. Chuo Kikuu cha Abuja aidha kinafunza shahada ndogo za uelekezi na kina Taasisi ya ualimu ili kushughulikia mahitaji ya wale ambao ni walimu kitaaluma, mahitaji maalum ya serikali mashirika ya elimu na hutoa nafasi ya ushirikiano katika masuala ya eleimu na mashirika vikundi mbalimbali ndani na nje ya Nijeriap.
Kwa sasa Chuo Kikuu cha Abuja kiko Gwagwalada kwa muda tu, Abuja, Nigeria kwenye ardhi ya ukubwa kiasi cha heka 11,824 ardhi ambayo inaendela kujengwa kando na barabara ya Kaduna-Lokoja-Abuja Road.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- tovuti rasmi Archived 11 Aprili 2010 at the Wayback Machine.
- Universities Socketworkers college Portal Archived 6 Oktoba 2008 at the Wayback Machine.
- Student portal Archived 28 Agosti 2008 at the Wayback Machine.