Chuo Kikuu cha Abraham Lincoln

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Chuo Kikuu cha Abraham Lincoln (kifupisho chake ALU kutoka Kiingereza Abraham Lincoln University) ni chuo kikuu cha mtandaoni kilichoko Los Angeles, California nchini Marekani. Wanafunzi huweza kuhudhuria masomo kwa njia ya intaneti au kwenda madarasani chuoni hapo.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Chuo Kikuu cha Abraham Lincoln kilianzishwa na Hyung J. Park mwanasheria wa masuala ya kodi aliyemaliza kusoma sheria kwenye Chuo Kikuu cha Loyola mwaka 1966. Park alikipa chuo hiki jina la Abraham Lincoln ambaye alikuwa rais wa Marekani kwa kuwa aijifunza sheria peke yake.

Taaluma[hariri | hariri chanzo]

Chuo kinatoa shahada, diploma na vyeti katika taaluma mbalimbali kama vile Sheria [1], Biashara na Teknolojia.[2]. Wanafunzi wana njia kadhaa za kusoma katika chuo hiki: kuhudhuria masomo darasani kwenye chuo hicho katika jiji la Los Angeles, kupia mtandaoni au mchanganyiko wa kupitia mtandaoni na kuhuduria masomo darasani.[3]


Abraham Lincoln University (ALU) and Abraham Lincoln University School of Law is an online university based in Los Angeles, California. Students may attend class in person or online.

Chuo Kikuu cha Abraham Lincoln kinatambuliwa na Distance Education Accrediting Commission.[4]. Hata hivyo Kitivo cha Sheria katika chuo hiki hakitambuliwi na American Bar Association na hadi mwaka 2017 wanafunzi wake hawaruhusiwi kuwa wanasheria katika majimbo 49 ya Marekani.[5][6]. ALU imesajiliwa na Committee of Bar Examiners of the State Bar of California kwenye kundi la vitivo vya sheria vya mtandaoni visivyotambuliwa.[7][8]

Wanafunzi wa kitivo cha sheria hupewa shahada ya J.D (Juris Doctor) na wanaruhusiwa kufanya mtihani kuwawezesha kuwa wanasheria katika jimbo la Califonia.[9]. Hadi Julai 2015, wanafunzi 386 walikuwa wamefanya mtihani wa California Bar Examination toka mwaka 1999 na wanafunzi 166 (43.0%) wamefaulu.[10]

Pamoja na kutoweza kuwa wanasheria majimbo mengine Marekani, wanafunzi wake wana njia kadhaa za kufanya kazi za sheria katika majimbo hayo.[11], Biashara na Teknolojia.[12]

Huduma kwa jamii[hariri | hariri chanzo]

Chuo Kikuu cha Abraham Lincoln hutoa huduma ya bure ya sheria kwa wanawake jijini Los Angeles. .[13] Law students are encouraged to volunteer.[14]. Chuo hiki pia hupunguza ada kwa wanafunzi ambao wamekuwa kwenye jeshi la Marekani. [15]


Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Nuvola apps bookcase.svg Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Abraham Lincoln kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.