Nenda kwa yaliyomo

Christian Doppler

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Christian Doppler

Christian Andreas Doppler (* 29 Novemba 1803 mjini Salzburg, Austria; † 17 Machi 1853 huko Venisi) alikuwa mwanahisabati na mwanafizikia Mwaustria.

Amekuwa maarufu kutokana na utambuzi wa athari ya Doppler iiyopokea jina lake.

Doppler alizaliwa Salzburg katika familia ya wachongaji wa mawe. Ilhali alikuwa mtoto mdhaifu hakujiunga na biashara ya familia bali aliruhusiwa kusoma. Alisoma kwenye chuo cha politekniki cha Salzburg akawa profesa msaidizi huko Prague iliyokuwa sehemu ya milki ya Austria wakati ule. 1836 alifunga ndoa na Mathilde Sturm. 1840 alipokelewa katika Shirika ya Sayansi ya Kifalme ya Bohemia na mwaka uliofuata alipewa nafasi ya kuwa profesa kamili kwenye Chuo cha Uhandisi Prague.

Alitunga kitabu kuhusu nuru yenye rangi ya nyota maradufu. Nadharia tete yake haikuthebitishwa lakini aliweza kuona athari ya Doppler kwenye mawimbi ya sauti; wakati wake reli za kwanza zilimwezesha kuonyesha mabadiliko ya sauti ya chanzo chenye kasi fulani.

Wakati wa mapinduzi ya 1848 alihamia Vienna akawa mkurugenzi wa taasisi ya fizikia ya Chuo Kukuu cha Vienna.

Baada ya kugonjeka kwenye mapavu alihamia Venisi (leo Italia) ka sababu ya tabianchi. Hapa aliaga dunia mwaka 1853.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: