Nenda kwa yaliyomo

Chevrolet Avalanche

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chevrolet Avalanche
2007 Chevrolet Avalanche LS
Kampuni ya magariGeneral Motors
ProductionSeptember 2001-April 2013
AssemblySilao, Mexico
ClassFull-size pickup truck
Body style(s)4-door pickup truck\
LayoutFront engine, rear-wheel drive / Four-wheel drive
Wheelbasein 130.0 (mm 3 302)
RelatedCadillac Escalade EXT
Chevrolet Suburban
DesignerMarc R. Asposito

Chevrolet Avalanche ni gari la Marekani aina ya pikapu inayo makao ya abiria 5 au 6 lenye milango minne na behewa la kubebea mizigo iliyotengenezwa na kampuni ya magari ya General Motors ya Marekani. Utengenezaji wa avalanche ulianzia Septemba 2001 na kutamatishwa Aprili 2013 ikiwa toleo la pili. Avalanche ilichukua muundo GM wa Chevrolet Suburban na Cadillac Escalade ESV wa kiunzi kirefu kati ya magurundumu.

Toleo la kwanza 2001–2006

[hariri | hariri chanzo]
Chevrolet Avalanche
1st Chevrolet
ProductionSeptember 2001 - December 2005
PlatformGMT805
Engine(s)
Transmission(s)
Marefu2002–03: in 221.7 (mm 5 631)
2004–06: in 221.6 (mm 5 629)
Upanain 79.8 (mm 2 027)
Urefu2002–03: in 73.3 (mm 1 862)
2004–06: in 73.6 (mm 1 869)
RelatedChevrolet Silverado/GMC Sierra
Chevrolet Suburban/GMC Yukon XL
Cadillac Escalade ESV
Cadillac Escalade EXT

Chevrolet Avalanche ilizinduliwa Septemba 2001 kama toleo lilonuiwa kutengenezwa 2002 chini ya GMT800. Mwaka wa kwanza Avalanche iliundwa na plastiki ya kijivu nyeusi kuitofautisha na Suburban/Yukon XL.

Avalanche ya kwanza ilikuwa na aina mbili za injini:

  • injini ya V8 ya Vortec ya lita 5.3 yenye nguvu ya 285 hp (216kW) na uzito wa nusu tani (1500 series)
  • Injini ya V8 ya Vortec ys lita 8.1 yenye nguvu ya 340 hp (253kW) na uzito wa tani robo tatu (2500 series)

Gari hili lilikuwa na mvuto mkubwa kwa uwezo wa kufunguka mlango uliogawa sehemu ya kubebea abiria na behewa la mizigo likiongezea sehemu ya kubebea mizigo. Viti vya abiria pia vilikuwa na uwezo wa kufungika kuongeza nafasi kwa dambra. Mwaka wa 2002 Chevrolet Avalanche iliteuliwa kwa tuzo kama SUV bora zaidi Amerika ya Kaskazini na jalida la Motor Trend iliishirikisha kama SUV ya mwaka.[1]

Chevrolet Avalanche Z71 ilikuwa na muundo na uwezo wa kutumika kwa barabara zisizo laini ilhali Z66 ilikuwa na muundo tu bila uwezo ikunuiwa kutumika kwa barabara laini.

Toleo la Pili 2007–2013

[hariri | hariri chanzo]
Chevrolet Avalanche
ProductionApril 2006–April 2013
Model year(s)2007–2013
PlatformGM GMT900 platform (Series GMT940: GMT941)
Engine(s)
Transmission(s)
Marefuin 221.3 (mm 5 621)
Upanain 79.1 (mm 2 009)
Urefuin 76.6 (mm 1 946)
Curb weight5,840 lb (2649 kg)
RelatedCadillac Escalade EXT
Cadillac Escalade ESV
Chevrolet Suburban/GMC Yukon XL
Chevrolet Silverado/GMC Sierra

Toleo ya pili ya Chevrolet Avalanche kwa jina GMT900 Avalanche ilizinduliwa Februari 2006 na utengenezaji rasmi ukaanza Aprili 2006 mjini Silao Mexico.

Sura ya GMT900 hasa mataa ya mbele ilifanana kwa ukaribu na yale ya Tahoe/Yukon na Suburban/Yukan XL. Gari hili pia lilihifadhi viti za abiria za kufunguka na ule mlango unaogawa sehemu ya kubebea abiria na behewa la mizigo sawa na toleo la kwanza.

GMT 900 ilizindua Z71 maalum toleo la pili la Z71 lenye ubora zaidi kwa matumizi kwenye barabara zisizo laini. Injini mpya ya V8 ya Vortec ya lita 5.3 inayotumia diseli oganiki E85. Injini hii mpya ilikuwa na nguvu ya 326hp (243kW), bora kuliko injini ya vortec ya lita 5.3 ya deseli ya hapo awali.

Aina za injini za toleo la pili (toleo la Black Diamond):-

  • V8 VortecMAX ya lita 6.0 (horsepower 367 (kW 274) (iliyozinduliwa 2006 - ikasitishwa 2010)

Umaarufu wa Cherolet Avalanche uliendelea na Michael Young mchezaji wa thamani zaidi 2006 wa baseboli alizawadiwa Avalanche ya 2007. Gari hili pia lilitumika kwa sinema mingi za Kimarekani has zenye zinahusishz uharifu kama vile CSI: New York. Kipindi cha ' Speed TV' Bullrun cha mwaka wa 2009 kiliorodhesha Avalanche Z71 nambali ya pili.

Hitimisho la utengenezai wa Chevrolet Avalanche

[hariri | hariri chanzo]

Aprili 2012, General Motors ilitangaza itaacha utengenezaji wa Avalanche mwaka uliofuata wa 2012 kufuatia kupungua kwa mauzo kwa 2.6% mwaka uliotangulia wa 2011.[2] GM iliendelea na utengenezai wa Cadillac Escalade EXT.

Magari yaliyouzwa Marekani

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Magari yaliyouzwa Marekani
2001[3] 52,955
2002[3] 89,372
2003[4] 93,482
2004[4] 80,566
2005[5] 63,186
2006[5] 57,076
2007[6] 55,550
2008[6] 35,003
2009[7] 16,432
2010[8] 20,515
2011[9] 20,088
2012 23,995
2013[10] 16,986
  1. "Motor Trend Trucks of the Year Winners List". Motortrend.com. 2009-02-24. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-09. Iliwekwa mnamo 2018-12-10.
  2. "GM announces end of Chevy Avalanche with Black Diamond edition". Autoblog. 13 Aprili 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Aprili 2012. Iliwekwa mnamo 2018-12-11. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 "GM Reports Best December Sales Since 1979". General Motors Media. Januari 3, 2003. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 23, 2009. Iliwekwa mnamo 2018-12-10. {{cite web}}: External link in |deadurl= (help); Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 "GM Reports December 2005 and Year Results". The Auto Channel. Januari 5, 2006. Iliwekwa mnamo 2018-12-10.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 "GM Reports 341,327 Deliveries In December". GM Communications. Januari 3, 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 23, 2009. Iliwekwa mnamo 2018-12-11. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 "GM Reports 221,983 Deliveries In December; 2,980,688 Vehicles Sold In 2008". GM Communications. Januari 5, 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 23, 2009. Iliwekwa mnamo 2018-12-13. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20090831002223/http://media.gm.com/servlet/GatewayServlet?target= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. http://media.gm.com/content/Pages/news/us/en/2010/Jan/0105_Dec_Sales/_jcr_content/iconrow/textfile/file.res/Deliveries%20December%2009.xls
  8. "December 2010 Sales: General Motors - Cheers & Gears Forums". Cheersandgears.com. Iliwekwa mnamo 2018-12-12.
  9. http://media.gm.com/media/us/en/gm/news.detail.html/content/Pages/news/us/en/2012/Jan/gmsales.html
  10. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-08-07. Iliwekwa mnamo 2018-12-16.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: