Nenda kwa yaliyomo

Cheez-It

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Cheez-Its)
Aina:
Kitafunio kaukau
Kampuni Inayomiliki:
Kampuni ya Kellogg(2001)
Ilipoanzishwa:
1921
Wamiliki wa hapo awali:
Kampuni ya Green & Green (1919)
Kampuni ya Sunshine Biscuits
(1929)
Kampuni ya Keebler(1996)
Tovuti Rasmi:
www.cheez-it.com/

Cheez-It ni kitafunio cha aina ya cracker Marekani kilichotayarishwa na kampuni ya Kellog. Kina vipimo vya 26 kwa 24 mm(1.0 kwa 0.95) na umbo la mstatili. Kimepikwa kwa kutumia unga wa ngano,mafuta ya mboga,jibini ya manjano,chumvi na viungo mbalimbali. Kuna aina mbalimbali za bidhaa za Cheez-It kama Cheddar Parmesan,Cheddar Jack,Party Mix na Hot & Spicy(iliyoundwa na Tabasco).Pia, wametayarisha cracker kubwa zaidi ya kuweza kutumbukizwa kwa mchuzi au kioevu ambacho mlaji anataka kutumbikiza ndani. Vitafunio hivi ni sawa na Kraft Cheese Nips.

Kulingana na rekodi za ofisi ya Marekani za usajili wa majina ya kibiashara ya bidhaa,vitafunio vya Cheez-It vya kwanza viliuzwa na Kampuni ya Green & Green wa Dayton,Ohio hapo Mei 1921. Baada ya shida za Wall Street za 1929,kampuni ya Green & Green ilinunuliwa na kampuni ya Sunshine Biscuits,iliyoanzishwa mwaka wa 1902 ikiitwa kampuni ya Loose-Wiles. Kampuni ya Keebler ilinunua Sunhine katika mwaka wa 1996 na Keebler,kwa upande mwingine, ukanunuliwa na Kampuni ya Kellog katika mwaka wa 2001. Vitafunio vya Cheez-It bado huuzwa chini ya nembo ya Sunshine.

Kitafunio cha Cheez-It kinavyofanana

Kaulimbiu ya kampeni ya zamani ilikuwa "Chukua pakiti yako mwenyewe" iliyopatikana kwenye pakiti nyingi. Upande mmoja wa pakiti ,pia, ulikuwa na "Anatomia wa Cheez-It." Katikati ya mwaka wa 2007,pakiti zilibadilishwa ili kuonyesha picha kubwa ya kipande cha jibini kilichoandikwa "Ladha yenyewe" huku picha ya Cheez-It ikikiinua kipande hicho cha jibini na kando yake kuandikwa "Ukubwa wenyewe". Kaulimbiu mpya ikichukua nafasi ya "Chukua pakiti yao mwenyewe" ilikuwa "Jibini Kubwa"("The Big Cheese").Jim Cummings akawa mtangazaji mpya wa matangazo yao ya televisheni.

Vilivyotumika kupika

[hariri | hariri chanzo]
  • Unga ulioongezwa virutubishi(unga wa ngano, niasini,chuma,thiamini,mononaitreti (vitamini B1), riboflavini (vitamini B2),asidi ya folic)
  • Mafuta ya mboga (kutoka mbegu za pamba, mafuta ya mitende, mafuta ya alizeti na kipimo kidogo cha mafuta ya soya na kuongezewa TBHQ)
  • maziwa jibini (maziwa , protini, viungo vya jibini, chumvi, rangi ya chakula ya annatto
  • chumvi
  • chachu
  • paprika
  • oleoresini (kuongeza rangi)[1] Archived 29 Machi 2010 at the Wayback Machine.
  1. http://www.cheez-it.com/cgi-bin/brandpages/product.pl?company=145
  2. http://www.oldtimecandy.com/cheez-its.htm Archived 3 Januari 2010 at the Wayback Machine.
  3. http://www2.kelloggs.com/brand/brand.aspx?brand=128 Archived 6 Machi 2009 at the Wayback Machine.
  4. http://www.zeer.com/Food-Products/Cheez-It-Baked-Snack-Crackers/000016687 Archived 29 Machi 2010 at the Wayback Machine.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]