Chasasa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chasasa ni mji wa wilaya ya Wete kisiwani Pemba.

Jina lina maana ya kitu cha muda uliopo, ila asili ni kuwa na nyumba zenye mtindo wa kisasa.

Mji huo una watu zaidi ya 3,000 kutokana na sensa ya mwaka 2012. Wenyeji wa mji huo ni watu waliohamia kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Vitongoji vya ndani ya mji huo ni kama vile: Kifumbikai, Mabandani, Ndovu, Sheli, Sudishabani, Jendele Kwa Bitii, Kwamapingu, Kwabuchi, Mkwajuni, pia Tangi ya Maji na Kwa Salum Rabia, Muhinani, Kwa Malimhilali.

Wakazi wa mtaa huu wana utamaduni wa ujirani mwema, Uislamu pia. Ni mtaa unaochangamka peke yake wakati wa usiku kwa bendi ya asili.

Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Pemba bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Chasasa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.