Nenda kwa yaliyomo

Central Depository and Settlement Corporation

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Central Depository and Settlement Corporation ama CDSC ni kampuni iliyobuniwa mwaka wa 2000 ili kuweka rekodi ya wamiliki hisa, uununuzaji na uuzaji wa hisa katika Soko la Hisa la Nairobi. Rekodi hii huwekwa kwa njia ya electroniki ili kurahisisha uununuaji na uuzaji wa hisa.

CDS ama "Central Depository System" ni mfumo wa kompyuta unaotomiwa na CDSC kuweka akaunti za hisa kwa njia ya kielectonik. Akaunti hizi huwa zimefunguliwa na wamiliki hisa kwa hivyo, mara kwa mara, CDS hutumika kubadilisha hisa kutoka akaunti moja hadi nyingine wakati hisa zinaponunuliwa na kuuzwa katika Soko la Hisa la Nairobi.

Hivyo basi, kila mmiliki hisa katika kampuni zilizosajiliwa katika Soko la Hisa la Nairobi ni lazima awe na akaunti ya CDS illi kuweza kushiriki katika kununua na kuuza hisa.

Unachohitaji kufunguwa Akaunti ya CDS

[hariri | hariri chanzo]

Ili kufungua akaunti ya CDS, unaitaji yafuatayo:

  • Picha mbili za paspoti zilizochukuliwa hivi karibuni
  • Kitambulisho cha taifa au Paspoti

Manuufa ya kuwa na Akaunti ya CDS

[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya manufaa ya kuwa na akaunti ya CDS ni kama:

  • Hisa hubadilishwa papo hapo wakati wa ununuzi na uuzaji
  • Kuepuka hatari zinazohusiana na ubadilishaji wa hati za hisa kama vile kuopte kwa hati au kupewa hati zisizo halali
  • Upungufu wa gharama ya ubadilishanaji wa hisa
  • Upungufu wa kazi na muda wa ubadilishanaji wa hisa
  • Kuwa na akaunti moja ya uwekezaji wa hisa, mafungo na mifumo mingine ya uwekezaji

Wamiliki wa CDSC

[hariri | hariri chanzo]
Mmiliki Asilimia
Capital Markets Challenge Fund Ltd 50.0%
Soko la Hisa la Nairobi 20.0%
ASK Nominees Ltd 18.0%
Capital Markets Investor Compensation Fund 7.0%
Uganda Securities Exchange Ltd 2.5%
Dar es Salaam Stock Exchange Ltd 2.5%

Angalia pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]