Cecil Kellaway

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Cecil Kellaway

Amezaliwa Cecil Kellaway
Agosti 22,1890
Afrika Kusini
Amekufa February 28,1973
Nchi Afrika kusini
Majina mengine Cecil Lauriston
Kazi yake Muigizaji


Cecil Kellaway(alizaliwa Agosti 22 1890 - akafariki Februari 28 1973)[1] alikuwa mwigizaji wa Uingereza / Afrika Kusini[2]. Aliteuliwa kuwania tuzo ya Academy Award for Best Supporting Actor kupitia filamu ya The Luck of the Irish na Guess Who's Coming to Dinner 1967.

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Cecil Kellaway alizaliwa Agosti 22 1890 huko Cape Town, Afrika Kusini. Alikuwa mtoto wa wazazi wa Kiingereza, Rebecca Annie (née Brebner) na Edwin John Kellaway, mbunifu na mhandisi. Edwin alihamia Cape Town kusaidia kujenga nyumba za bunge pale Cape Town na alikuwa rafiki mzuri wa Cecil Rhodes, ambaye alikuwa baba wa ubatizo wa Cecil..[3]

Cecil alivutiwa na uigizaji tangu akiwa mdogo.[4] Alisomeshwa katika chuo cha Normal, Cape Town na huko England katika shule ya Grammar. Alisomea uhandisi na aliporudi Afrika Kusini aliajiriwa katika kampuni ya uhandisi. Walakini hamu ya uigizaji ilikuwa kali sana na alikua muigizaji wa wakati wote, akiigiza kwanza katika filamu "Potash na Perlmutter.[3][5][6]

Alitumikia kwa muda mfupi jeshini mnamo 1914 lakini alitolewa nje.[7] Filamu ya mapema aliyoigiza ilijulikana kama The Prince of Pilsen.

Alifanya ziara kwa miaka mitatu kupitia China, Japan, Siam, Borneo, Malaya, Kaskazini na Afrika Kusini na Ulaya, katika filamu kama "Monsieur Beaucaire".

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Cecil Kellaway kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Kellaway, Cecil Lauriston (1890–1973)". Kellaway, Cecil (1890–1973). Australian Dictionary of Biography (Australian National University). Iliwekwa mnamo 1 June 2011.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. Obituary, Variety, 7 March 1973, page 78.
  3. 3.0 3.1 "GREENROOM GOSSIP", 27 August 1931, p. 16. 
  4. "THE KELLAWAY FAMILY ON STAGE AND SCREEN", 4 August 1938. 
  5. "Character Actor Cecil Kellaway is Dead at 79.", 1 March 1973. 
  6. "The THEATRE & its PEOPLE", 17 July 1924, p. 21. 
  7. "Round the Shows", 30 July 1925, p. 2.