Nenda kwa yaliyomo

Catherinerose Barretto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Catherinerose Barretto
Nchi Mtanzania
Anafahamika kwa Mwanzilishi Mwenza KINU innovation Hub
Ndoa Ameolewa
Mahusiano John Paul Barretto (Kaka)
Wazazi Tony Barretto (Baba), Pearl Carvalho Barretto (Mama)


Catherinerose Barretto ni mwanzilishi mwenza wa kampuni za Pamoja Initiative Ltd (inayohusika na mambo ya ajira, uteuzi, mafunzo na ushauri), Binary Institute of Technology[1], KINU group of Companies ambayo inafahamika zaidi kwa kuwa moja ya hatamizi binafsi za mwanzo zilizo jihusisha na mambo ya teknolojia na biashara nchini Tanzania iliyofahamika kwa jina la KINU Innovation Hub. [2]

Elimu yake

[hariri | hariri chanzo]

Mama mzazi wa Catherine alikuwa ni mwalimu katika shule ya kimataifa ya International School of Tanganyika (IST) aliye fahamika kwa jina la Pearl Carvalho Barretto na baba yake ni Anthony Edgar Barretto maarufu kama Tonny Baretto ambaye alikuwa mmoja wa waandishi na aliyewahi kuwa msimamizi wa kampuni ya kuchapisha magazeti ya serikali iitwayo Tanzania Standard Newspapers Limited (TSL) yenye kuchapisha magazeti kama Daily News, Habari Leo na Sunday News. [3]

Catherine alisoma katika shule ya International School of Tanganyika na baadaye akaenda kusoma Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha California State University Fresno na baadae akasomea kozi ya Maendeleo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam[4].

Kuanzia miaka ya 2011 mara baada ya kuanzishwa kwa Kampuni yao ya KINU group of Companies, kupitia Hatamizi yao ya KINU Innovation hub iliyo anzishwa na watu sita wakiweno Emmanuel Feruzi, Luca Neghesti (mmiliki na mwanzilishi wa Bongo5), Johnpaul Barretto, Jones Mrusha na Taha Jiwaji (Mwanzilishi wa BongoLive na Beem Catherine amekuwa ni Mwanamke mwenye mchango mkubwa katika ustawi wa biashara zinazo chipukia na zenye kutumia TEHAMA kama nyenzo.[5]

Amekuwa ni mshiriki katika mipango inayo husisha maendeleo ya rasilimali watu, ujasiriamali na kujenga uwezo ndani ya jumuiya ya TEHAMA na mambo ya kibunifu.

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-03-14. Iliwekwa mnamo 2024-03-14.
  2. "Catherinerose Barretto | WSA" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-03-14.
  3. "Swahili Time". swahilitime.blogspot.com. Iliwekwa mnamo 2024-03-14.
  4. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/national/catherinerose-we-shouldn-t-be-gatekeepers-but-door-openers-4452690
  5. https://michuzi-matukio.blogspot.com/2012/09/official-opening-of-kinu-innovation.html