Nenda kwa yaliyomo

Carl Ross

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'

Carl Ross
Uuzaji wa samaki huko Tokyo, 2002
Amezaliwa29 Julai 1901
Amefariki9 Januari 1986
Kazi yakemfanyibiashara wa samaki


(John) Carl Ross (Cleethorpes, Lincolnshire, Uingereza, 29 Julai 1901 - Grimsby, 9 Januari 1986) alikuwa mfanyabiashara wa samaki aliyefanikiwa sana. Alikuwa mwanzilishi wa kampuni iliyokuja kuwa Young's Bluecrest, inayoongoza katika sekta ya uuzaji wa samaki waliohifadhiwa nchini Uingereza.

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Alikuwa mwana wa nne katika watoto sita wa Thomas Ross, mwanzilishi wa kampuni ya kuuza samaki ya Ross. Carl Ross alisoma katika Shule ya Culford (alikocheza mpira wa magongo) na akafanya kazi na Kikosi cha Jeshi la Wanamaji kabla ya kuhusika katika biashara ya familia katika mwaka wa 1918 alipotoka jeshi. Thomas alistaafu mapema katika mwaka wa 1928 na kutoka hapo Carl akawa mkuu wa kampuni ya familia. Carl aliingia na mipango na mawazo mapya kama kununua samaki waliohifadhiwa katika barafu kutoka Amerika ya Kaskazini - hii ilisababisha upanuzi wa biashara yao baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Kazi yake

[hariri | hariri chanzo]

Ross alipokuwa akijenga biashara ya uuzaji wa samaki,alitambua kuwa mustakabali ya sekta iliyohusu samaki ilikuwa katika kuunganisha michakato ya uvuvi , usindikaji na uuzaji wa samaki.Hivyo basi,akaunda mashua ya mafuta ya dizeli ya kwanza katika miaka ya 1930. Yeye alinunua mashua tisa katika mwaka wa 1943 na kununua hisa nyingi kabisa katika kampuni ya kuunda mashua ya Trawlers Grimsby Ltd, katika mwaka wa 1944. Hii ilikuwa msingi wa lile lilichokuja likawa Kundi la Ross.

Kulingana na makala ya gazeti la The Times (14 Januari 1986) alikuwa bila masomo yoyote rasmi katika uhasibu, Ross alionyesha talanta kubwa katika kuelewa na kusoma hesabu na akapata heshima nyingi katika jiji lao. Kubadilika sana kwa usimamizi kwa kampuni zilizohusika na sekta ya kuvua na kuuza samaki huko mji wa Hull kulipea Kundi la Ross soko zuri huko Humber.

Mwanzoni mwa miaka ya 1950, Carl Ross alitambua kwamba sekta ya samaki imo katika ya sekta ya chakula, yeye alipanua biashara ya Kundi la Ross kutoka uuzaji wa samaki pekee na kuwa Kundi la Ross Foods. Aliongeza sehemu nyingine katika biashara ya Ross Foods aliponunua Kampuni ya Young Shellfish.

Katika mwaka wa 1956,Ross aliweza kuajiri nahodha ishirini bora katika eneo la North Sea na mpango wake wa kuunda mashua ya madaraja ya Bird na Cat ulikuwa na mafanikio mengi sana. Rekodi ya faida ya vyombo vya maji vya Ross vikajulikana na kundi hilo likajenga vyombo vingine vingi sana hapo Selby.

Carl Ross alianzisha Ross Poultry,iliyokuwa muhimu sana katika kuanzisha msingi wa biashara ya aina hiyo huko Uingereza.Akaunda kampuni kubwa kabisa ya kusambaza viazi nchini Uingereza na akaanzisha kampuni mbalimbali kama Ross Motorway Services (1965).

Katika ukuaji wa haraka wa Kundi la Ross, kikwazo kilikuwa kimoja tu katika mwaka wa 1966, Tume ya Monopolies ilimkataza kununua Associated Fisheries, kampuni nyinge maarufu katika sekta ya uuzaji samaki.

Carl Ross aliachana na kampuni yake baada ya mgogoro katika bodi,hapo mwisho wa miaka ya 1960. Ingawa alikuwa akikaribia umri wa miaka sabini, yeye alienda na kuwa mwenyekiti wa kuendeleza kampuni ya Cosalt plc ya kuendeleza vifaa vya marina. Aliendelea kujihusisha na masuala ya kampuni hiyo hadi alipokufa.

Maisha ya binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Ross alikuwa amemwoa Elsie Hartley, binti ya mfanyibiashara wa pamba wa Blackburn katika mwaka wa 1928. Walikuwa wana wawili na mabinti wawili. Alifurahia mchezo wa kupiga risasi na alimiliki farasi za mbio kadhaa. Alipata kibali cha kuwa rubani wa ndege na akajihusisha katika kundi la kujitolea ya Royal Air Force Volunteer Reserve katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Miongoni mwa tuzo nyingine alikuwa rais wa zamani na mwanachama wa Muungano wa Sekta ya Uuzaji Samaki wa Michezo.Alikuwa karimu sana huku akitoa udhamini katika vituo vingi vya misaada. Alikuwa rais wa Chama cha Kihafidhina cha Grimsby kwa miaka ishirini na mitano kuanzia mwaka wa 1954.

Mjukuu wake ni David Ross, mwanzilishi mshiriki wa kampuni ya kuuza simu za mkono, Carphone Warehouse, akiwa na mali ya takriban £ 312m.

Angalia pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  • Ripoti juu ya kundi la Ross Archived 28 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
  • Bendera za mashua ya Kundi la Ross Archived 30 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
  • Matthew, H.C.G. (2004). Oxford Dictionary of National Biography. Oxford University Press. ISBN 978-0198614111.