Nenda kwa yaliyomo

Kundi la Ross

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo la Grimsby katika ramani. Makao makuu ya Kundi hili

Kundi la Ross ni kampuni ya Uingereza iliyoanzishwa Grimsby, Uingereza katika mwaka wa 1920 na Thomas Ross.Kampuni hii iliendelea na kuwa wajibu wa mwana wake Thomas ,(John) Carl Ross baada ya kustaafu kwa Thomas hapo 1928. David Ross,alikuwa mwanzilishi na mwenye hisa nyingi katika shirika la kuuza rununu,Carphone Warehouse, ni mjukuu wa J.Carl Ross.

Operesheni

[hariri | hariri chanzo]

Hapo mwanzoni

[hariri | hariri chanzo]

Hapo mwanzoni,ilikuwa kampuni ndogo ya familia ya kuuza samaki lakini ikaendelezwa na Ross ikawa ya kuvua na kusindika samaki.Baadaye wakaingia katika kusindika chakula kwa jumla. Kampuni ilinunua mpinzani wake wa Kibiashara,Young's,katika mwaka wa 1959.Baada ya muungano kadhaa na kubadilika kwa usimamizi mara kadhaa, hii ndiyyo inayounda kampuni iitwayo sasa Young's Bluecrest, kiongozi(Uingerza) katika sekta ya samaki waliohifadhiwa katika barafu. Jina la Ross linabakia kuwa ya kawaida katika uuzaji wa samaki waliohifadhiwa kwenye barafu.

Ilipofika Vita ya Pili ya Dunia,kampuni hii ilikuwa ikiendesha biashara ya samaki katika matawi ya Leeds,leicester na Fleetwood na ,vilevile, makao yao ya Grimsby.

Walianza na meli nne za kuvua samaki katika miaka ya 1930s,Kundi la Ross lilipanua mipango yao na kununua meli kubwa zaidi za uvuvi. Upataji wa hisa kubwa katika Trawlers Grimsby katika mwaka wa 1944 ikifuatiwa na ununuzi wa vikundi kadhaa vya mashua ya uvuvi kama Kampuni ya Queen Steam Fishing. Carl Ross,katika mwaka wa 1956,walinunua kampuni ya G F Sleight,iliyoajiri nahodha 20 bora nchin Uingereza, na kundi lao likaanza kuunda meli katika kampuni yao ya Cochrane Shipyards ya Selby. Waliunda aina mbili maarufu zilizojulikana kama daraja la Cat na la Bird. Katika mwaka wa 1960 / 1, kundi la Ross lilinunua kampuni ya Rinovia Steam,Walipokuwa wamefanikiwa sana,kundi hili lilikuwa na mkusanyiko mkubwa kabisa wa mashua ya uvuvi katika Bara Uropa. Kampuni ilinunua pahala pa kuunda meli, na ikaanza kuunda meli zao wenyewe.

Mwanzoni mwa miaka ya 1960,Kundi la Ross lilikuwa na biashra mbalimbali kama kuku na ndege,vyakula vilivyofifadhiwa kwa barafu kama samaki,pamoja na,uvuvi ,uuzaji wa samaki na operesheni nyingine mbalimbali. Ingawaje,operesheni za uvuvi za kampuni \,zilizowakilisha asilimia 5 tu ya mauzo, zilianza kuleta hasra mwaka baada ya mwaka.

Carl Ross alitoka kundi hilo baada ya vita katika bodi ya wakurugenzi na ,matokeo ya moja kwa moja ya hii,Imperial Tobacco ilichukua usimamizi wa kundi. Carl Ross alipokuwa akiongoza kundi hilo la Ross , kampuni ilipanuka na kuingia bashara ya bidhaa zisizo samaki. Wakati kampuni zisizohusika na biashara ya samaki zilikuwa na kubadilika kwa usimamizi, vikundi vya mashua ya Kundi la Ross vilichukuliwa na British United Trawlers.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]