Calgary Sun

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Calgary Sun
Jina la gazeti Calgary Sun
Aina ya gazeti *. Gazeti la kila siku
Lilianzishwa 1980
Eneo la kuchapishwa Calgary
Nchi Kanada
Mmiliki Kampuni ya Sun Media(Kampuni shirika ya Quebecor)
Makao Makuu ya kampuni Calgary, Alberta
Machapisho husika *. 24 Hours
Tovuti Calgary Sun

'Calgary Sun ni gazeti la kila siku linalochapishwa katika eneo la Calgary, Alberta Kanada. Hii ni mgawanyiko wa Sun Media, kampuni ya Quebecor.

Lilichapishwa kwa mara ya kwanza katika mwaka wa 1980, gazeti hili huchapishwa katika mtindo sawa na tabloid na lilichukua nafasi ya gazeti la hapo awali,The Albertan, baada ya kununuliwa na wachapishaji wa Toronto Sun.

Gazeti hili, kama mengine yote ya kampuni ya Kanada ya Sun, linajulikana kwa makala fupi ya habari yanayolenga wasomaji wanaofanya kazi. Mpangilio wa makala katika Sun hufanana , kwa kiasi fulani, na magazeti ya porojo ya Uingereza.

Vipengele[hariri | hariri chanzo]

Ukurasa wa sita[hariri | hariri chanzo]

Ukurasa wa sita, tangu zamani,umekuwa wa "uvumi" au matukio yaliyofanyika yaliyochekesha/ maoni kuhusu matukio. Hivi sasa,Ukurasa wa Sita unaandikwa na Kelly Doody, mwanamichezo wa kuogelea wa zamani wa timu ya taifa ya Kanada.

Sunshine Girl[hariri | hariri chanzo]

Kipengele hiki ni maarufu katika gazeti la Calgary Sun - kama magazeti mengine ya mnyororo wa Sun- na huwa na picha maridadi ya mwanamke yeyote anayefanya kazi za kupigwa picha za matangazo au za kutangaza nguo mpya kwa umma. Mwanamke huyu ndiye anayeitwa Sunshine Girl. Kipengele hutumia picha za wanawake wa nchi hiyo zilizopigwa na wataalam au za kupigwa na watu wenyewe ama ,pia, zinazopigwa na gazeti lenyewe. Hapo awali, kilikuwa katika ukurasa wa 3 (kama magazeti ya Uingereza ambayo Sun lilitaka kuiga yalikuwa na picha kama hizi katika ukurasa wa 3) lakini katika miaka ya 1990 kilihamishwa hadi sehemu ya habari za michezo. Kipengele cha Sunshine Boy cha wanaume kilichapishwa katika miaka ya 1980 na 1990.

Magazeti ya kila wiki[hariri | hariri chanzo]

Kwa miaka mingi, Calgary Sun ,pia, lilichapisha gazeti maarufu la kila wiki ,Calgary Mirror, lililohusisha habari za jamii; shirika la Sun likanunua gazeti hili katika mwanzoni wa miaka ya 1990. Chapisho hili, ambalo lilianza katika miaka ya 1950 na lilijulikana kama North Hill News, liliacha kuchapishwa katika mwaka wa 2001. Nafasi yake ilichukuliwa na FYI Calgary In-Print, gazeti la bure la kila wiki lililolengwa kuwa chapisho la tovuti ya Sun habari ya FYI Calgary (kulikuwa na gazeti la FYI Toronto lililokuwa chapisho la tovuti ya Toronto Suns).Chapisho jipya lilishindwa kuvutia wasomaji na watangazaji na likaacha kuchapishwa katika mwezi wa Mei 2001 katika operesheni za kupunguza ukubwa wa kampuni ya Sun Media. Tovuti iliachisha dhana ya FYI mwaka mmoja baadaye na kujiita Calgarysun.com.

Mtindo[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 2 Oktoba 2006, Sun lilibadilisha mtindo wake kwa njia kubwa hasa likianzisha nembo mpya (nembo hii ilikuwa imetumika na magazeti mengine ya Sun kwa miaka kadhaa) na ,pia, kubadilisha njia ya uchapishaji wa makala na vichwa vya habari. Mnamo Februari 2007, Sun Media ilizindua toleo la eneo la Calgary la gazeti lake la bure, 24 Hours, linalotumikwa na wafanyikazi wa Calgary Sun.

Usambazaji[hariri | hariri chanzo]

Calgary Sun ni mojawapo ya magazeti manne ya kila siku yanayopatikana katika eneo la Calgary. Gazeti la pili ni Calgary Herald. La tatu na la nne ni Metro News na Rush Hour News. Usambazaji unafanyika kwa kuagiza, mauzo ya moja kwa moja( kwa mfano katika maduka) ama kwa kutumia masanduku ya magazeti. Mtindo huo wa masanduku ya magazeti ulileta mjadala mkali kutoka Halmashauri ya Jiji katika mwanzo wa mwaka wa 2008 baada ya kiongozi mmoja kudai kuwa masanduku hayo yalisababisha maongezeko ya takataka.

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]