Business Line
Business Line | |
---|---|
Jina la gazeti | Business Line au The Hindu Business Line |
Aina ya gazeti | *. Gazeti la lugha ya Kiingereza *. Gazeti la kila siku |
Lilianzishwa | 1994 |
Eneo la kuchapishwa | Bangalore, Chennai, Coimbatore, Delhi, Hyderabad, Kochi, Kolkata, Madurai Mangalore, Mumbai, Thiruvananthapuram, Tiruchirapalli, Vijayawada na Visakhapatnam. |
Nchi | Uhindi |
Mhariri | *. Bw. N. Ram *. Bw. K Venugopal |
Nakala zinazosambazwa | 130,000 Nakala nyingi husambazwa Jumapili |
Machapisho husika | *. eWORLD *. Smartbuy *. BrandLine *. Life |
Tovuti | Tovuti Rasmi |
Business Line au The Hindu Business Line ni gazeti la kibiashara la Kihindi linalochapishwa na Kasturi & Sons ambao huchapisha ,pia, gazeti la The Hindu. Hili ndilo gazeti jeupe tu katika biashara.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Business Line lilianza kuchapishwa katika mwaka wa 1994. Huchapishwa kwa mtindo wa gazeti pana na huwa na usambazaji wa nakala takriban 130,000. Nakala za Business Line husambazwa sana katika siku ya Jumapili kulik siku zingine.
Business Line huchapishwa katika maeneo 14:Bangalore, Chennai, Coimbatore, Delhi, Hyderabad, Kochi, Kolkata, Madurai, Mangalore, Mumbai, Thiruvananthapuram, Tiruchirapalli, Vijayawada na Visakhapatnam.
Mhariri mkuu ni Bw. N. Ram na Mhariri Mshiriki ni Bw. K Venugopal. Mwandishi Mohan Padmanabhan huandika makala mengi katika gazeti hili.
Wafanyakazi wake wengi ni waandishi na watafiti. Hili ndilo gazeti pekee lililo na sehemu ya utafiti.
Vipengele
[hariri | hariri chanzo]Jumanne hadi Jumamosi
[hariri | hariri chanzo]Kutoka Jumanne hadi Jumamosi, sehemu kuu ya Business Line ina kurasa 20 - 24. Vichwa vya kurasa ni kama Corporate(Kampuni), Information Technology(Teknolojia ya Mawasiliano), Marketing(Masoko),Editorial & Opinion(Makala ya Mhariri & Maoni) - kurasa mbili, Commodities & AgriBusiness(Bidhaa & Biashara ya Ukulima),Economy(Uchumi), International Business(Biashara ya Kimataifa), Stock Market News(Habari za Soko la Hisa), Stocks & Mutual Fund (kurasa tano), States Variety ,Logistics na Market Watch.
Jumapili
[hariri | hariri chanzo]Jumapili,sehemu kuu ya Business Line ina kurasa 18. Vichwa vya kurasa ni kama Economy(Uchumi),Commodities(Bidhaa),Corporate(Kampuni), International(Kimataifa),Variety, Young Investor(Mwekezaji kijana) na Investment World(Dunia ya Uwezekaji) - kutoka ukurasa wa 8 hadi ukurasa wa 17(mawaidha kuhusu hisa , fedha na amana).
Jumatatu
[hariri | hariri chanzo]Jumatatu,sehemu kuu ya Business Line ina kurasa 16. Vichwa vya kurasa ni kama Market Mood(hali ya Masoko),EconomyUchumi, Information Technology(Teknolojia ya Mawasiliano),AgroBusiness(Biashara ya Ukulima), Transport(Usafiri),'Commodities Investment(Uwekezaji wa Bidhaa), New Manager(Meneja Mpya) - hufahamisha kuhusu viongozi katika dunia ya biashara, Mentor - hufahamisha watu kuhusu kodi, mifumo ya biashara na vitabu, Money & Banking(Pesa na Benki), Editorial & Opinion(Maoni ya Mhariri na Maoni) na States(Majimbo) na Variety.
Machapisho shirika
[hariri | hariri chanzo]Jumatatu | eWORLD |
Jumatano | Smartbuy |
Alhamisi | BrandLine |
Ijumaa | Life |
Kwenye mtandao wa tarakilishi
[hariri | hariri chanzo]Tovuti ya BUSINESSLINE Online ilianzishwa kwenye mtandao katika mwezi wa Juni 1995. Kurasa za tovuti hii huangaliwa mara milioni 14 kila mwezi duniani kote. Misemo ya Sensex kwenye ukurasa wa kwanza huvutia wengi.
Bei
[hariri | hariri chanzo]Gazeti hili huuzwa kwa bei ya rupia 4 ($0.10) ya Kihindi katika siku za Jumatatu hadi Jumamosi na bei ya Jumapili ni rupia 3 ($0.075). Magazeti mengine kama The Economic Times na The Financial Express huuza bei sawa katika matoleo yao ya Jumamosi na Jumapili (rupia 7 - rupia 10).Business Line limekuwa na bei sawa wiki nzima isipokuwa Jumapili. Magazeti mengine kama Mint na Business Standard hayachapishwi Jumapili.