Nenda kwa yaliyomo

Bunge la 10 la Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bunge la 10 la Jamhuri ya Kenya lilifunguliwa 15 Januari 2008, likiwa na kundi la Orange Democratic Movement likiongozwa na Raila Odinga, likiwa na wajumbe wengi zaidi. Raila alikuwa mgombea urais katika uchaguzi wa 2007, ambao ulisababisha utata wa ushindi kwa Mwai Kibaki wa PNU. Mwanachama wa ODM, Kenneth Marende alichaguliwa kama spika wa bunge la 10, akamshinda mwanachama wa PNU Francis ole Kaparo 105-101 katika raundi ya tatu ya kura.

Ufunguzi wa bunge ulikuwa na utata mwingi; Mwai Kibaki alikaribishwa na wanachama wa ODM kwa unyamavu mwingi na kuzomewa, Raila naye alikaribishwa na shutuma za mauaji.

Uzinduzi wa Bunge la 10 ulikuwa 6 Machi 2008, wakati Odinga aliapa kuwa Waziri Mkuu na kielezo cha National Accord and Reconciliationcha 2008 kupitishwa.

Vipindi na Bili zilizopitishwa

[hariri | hariri chanzo]

21 Aprili 2009 - Bunge lafunguliwa. Msuguano kati ya Rais na Waziri Mkuu ulitokea wakati wote waliwasilisha barua zao kwa Spika za mapendekezo yao ya Kiongozi wa Biashara ya Serikali (Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara ya Bunge). Spika hatimaye alifanya uamuzi wake na alijiwakilisha kama mwenyekiti hadi msuguano ulipotatuliwa.

30 Aprili 2009 - Bunge yaidhini orodha ya IIECK (Interim Independent Electoral Commission of Kenya) ambayo ingesimamia uchaguzi ujao.

7 Mei 2009 - Bunge yaidhini orodha ya IIBRCK (Interim Independent Boundaries Review Commission of Kenya) ambayo ingeangalia mipaka ya jimbo na wilaya ili kuhakikisha kuwa ni wawakilishi halisi zaidi ya idadi ya watu kulingana na takwimu za usajili wa wapigakura au hesabu za watu wote za 2009 ambayo inafaa kumalizika mwezi Oktoba 2009. Siku iyo hiyo, Rais Kibaki alikubali bili iliyoumba IIECK na akateuwa rasmi makamishna wa IIECK.

12 Mei 2009 - Rais Kibaki alikubali bili iliyoumba IIBRCK na akateuwa rasmi makamishina waliyoidhinishwa na Bunge.