Nenda kwa yaliyomo

Kenneth Marende

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Spika, Lok Sabha, Smt. Meira Kumar akutana na Spika wa Bunge la Kenya, Bwana Kenneth Marende, EGH, wakati wa Mkutano wa 56 wa Jumuiya ya Wabunge wa Jumuiya ya Madola, huko Nairobi, Kenya, mnamo Septemba 14, 2010.

Kenneth Otiato Marende alikuwa Spika wa Bunge la kumi nchini Kenya. Alichaguliwa kama Spika wa Bunge manamo tarehe 15 Januari 2008.

Katika duru ya kwanza ya kupiga kura, Marende, ambaye alikuwa mgombeaji wa chama cha "Orange Democratic Movement" (ODM) kwa nafasi ya Spika, alipata kura mia moja na nne, wakati mgombeaji wa serikali, Francis ole Kaparo, alipata kura tisini na tisa; katika duru la pili Marende alipata kura mia moja na nne na Kaparo alipata mia moja na mbili. Ingawa wengi wao mara ya kwanza walitaka duru mbili, hatimaye kidogo tu ndio ilikuwa inahitajika, na Marende alichaguliwa katika raundi ya tatu kwa kura mia moja na tano dhidi ya mia moja na moja kwa Kaparo.

Muda wake wa kwanza alichaguliwa kama mbunge kwa Emuhaya Constituency kwenye tiketi cha chama cha NARC katika uchaguzi wa mwaka 2002. Alibaki kwenye kiti chake katika uchaguzi wa mwaka wa 2007, lakini uchaguzi wake kama Spika ilimaanisha ya kuwa kiti chake iliachwa wazi, uchaguzi mwingine baina yake ilistahili kufanywa. Uchaguzi mwingine ukafanyika mwezi wa Juni 2008 na Wilbur Ottichilo aliibuka mshindi wa chama cha ODM.

Katika Bunge la tisa aliuunga mkono marekebisho kwa mswaada kwa ubakaji kwa ndoa. Alisema kwa maarifa kwenye sakafu ya Bunge kuwa "WaKenya bado wanaweza kufanya mapenzi na wenzao hata wanapokuwa wamelala ila tu wawe wameoana."

Mwezi wa Aprili 2009, wakati bunge ilipofunguliwa tena, alikuwa amelazimishwa kufanya tawala ya uzito juu ya nani atakayekuwa Kiongozi wa Serikali ya Biashara kutokana na mzozano baina ya Rais na Waziri Mkuu. Katika tawala ya kihistoria, yeye alijipatia mda maalum, kwa kuzingatia maagizo ya bunge kusimama kama Mwenyekiti wa Kamati la Biashara mpaka kutatuliwa.

Ofisi za Kisiasa
Alitanguliwa na
Francis ole Kaparo
Spika wa Bunge la Kenya
2008–present
Incumbent
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kenneth Marende kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.