Nenda kwa yaliyomo

BrooWaha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya BrooWaha
BrooWaha
Mfano wa ukurasa katika BrooWaha
Jina la gazeti BrooWaha
Aina ya gazeti Gazeti Kwenye mtandao wa tarakilishi
Lilianzishwa Septemba 2006
Eneo la kuchapishwa Los Angeles, New York, San Francisco
Atlanta Houston na Miami
Nchi Marekani Marekani
Mwanzilishi BrooWaha LLC
Mhariri David Cohn [1]
Mmiliki BrooWaha LLC
Tovuti http://www.broowaha.com/

BrooWaha ni gazeti la raia kwenye mtandao wa tarakilishi linaloripoti sana habari za eneo lake la Los Angeles. Makala zinazochapishwa kwenye tovuti yameandikwa na watumiaji wake pekee.

Matoleo kadhaa ya BrooWaha yameanzishwa katika majiji makuu ya Marekani kama Los Angeles, New York, San Francisco na hivi majuzi kabisa, Atlanta, Houston na Miami. Habari zote za matoleo haya huonyeshwa katika tovuti kuu ya BrooWaha.

Tovuti hii ilionyeshwa katika gazeti la Los Angeles Times katika mwezi wa Desemba 2006.

Watumiaji waliosajiliwa katika tovuti ya BrooWaha huwa na ruhusa ya kuandika makala kwenye ukurasa maalum ya maandishi katika tovuti. Ukurasa huu huwezesha watumiaji kuandika makala na kuambatanisha picha na kuyawasilisha kwa wahariri. Makala, kwa kawaida, huchapishwa katika au baada ya saa 24. Licha ya kuwapa watumiaji chaguo nyingi za kuandika maandishi kwa njia mbalimbali, tovuti hiyo imepata umaarufu wa kuweza kuwa na viungo vya tovuti zingine na huonyesha video ya YouTube katika makala yao.

Wahariri

[hariri | hariri chanzo]

Jukumu la wahariri wa BrooWaha ni dogo sana na hasa huwa kuthibitisha kuwa makala haya hayana ubaguzi au habari zozote zisizotakikana.. Tangu mwanzo wa mwaka wa 2008, tovuti hii imehaririwa na David Cohn [2] Ilihifadhiwa 30 Mei 2021 kwenye Wayback Machine..

Ukurasa wa maoni ni kipengele maarufu cha BrooWaha. Majadiliano huonekana sana kati ya mwandishi wa makala na wasomaji wa makala katika kipengele hiki cha maoni. Mbali na kupigia kura makala, wasomaji huweza kupigia kura maoni ya watu wengine ili kuhimiza majadiliano mazuri.

Umaarufu

[hariri | hariri chanzo]

Watumiaji wa BrooWaha hupokea 'pointi za umaarufu' kulingana na idadi ya makala wanayoandika na umaarufu wa makala yao. Jumla ya pointi hizi inaathiri cheo chao katika shirika la gazeti hili. Makala ya watumiaji maarufu sana huonyeshwa zaidi kwenye tovuti na wao huwa na uzito zaidi wanapopiga kura kwa makala ya wengine.

Marafiki

[hariri | hariri chanzo]

Watumiaji wa BrooWaha huweza kuongeza waandishi wa habari wanaowapenda kama marafiki yao na kuarifiwa wanapoandika makala kwa kuwatumia ujumbe kwa anwani yao kwenye mtandao.

Mkahawa wa BrooWaha

[hariri | hariri chanzo]

Kila toleo la BrooWaha huwa na ukurasa wa majadiliano unaoitwa BrooWaha Cafe (Mkahawa wa BrooWaha) ambapo watumaji hujadiliana kuhusu mada mbalimbali kutoka porojo hadi habari motomoto zilizofanyika.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]