Bioko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Bioko
Pwani ya Arena Blanca, Kisiwa cha Bioko

Bioko ni kisiwa kilichopo kilomita 32 mbele ya pwani ya magharibi ya Afrika katika Ghuba ya Guinea. Ni sehemu ya kaskazini kabisa ya nchi ya Guinea ya Ikweta.

Kisiwa kilikadiriwa kuwa na wakazi 297,000 kwenye mwaka 2019[1]. Eneo la Bioko lina jumla ya km2 2017. Kisiwa kina urefu wa km 70 kikiwa na upana wa km 32. Kilele chake cha juu zaidi ni Pico Basile inyofikia mita 3012 juu ya UB.

Mji mkubwa ni Malabo, upande wa kaskazini ya kisiwa. Malabo ni mji mkuu wa kitaifa wa Guinea ya Ikweta.

Kiutawala Bioko imegawiwa kwa mikoa miwili ya Bioko Norte na Bioko Sur

Marejeo[hariri | hariri chanzo]