Nenda kwa yaliyomo

Betri ya gari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Betri ya gari (kwa Kiingereza: Automotive battery) ni betri inayoweza kuchajiwa ili ilipatie gari nguvu za kielektroniki. Haswa, betri ya gari husaidia injini kuwaka. Injini ikishanguruma na kuanza, basi gari hupata nguvu kutoka altaneta.

Historia ya betri za gari

[hariri | hariri chanzo]

Hapo kitambo, hakukuwa na betri za gari. Injini ziliweza kuanzishwa na uzio uliojulikana kama crank kwa lugha ya Kimombo. Gari hazikuhitaji nguvu za kielektroniki maana kengele ilitumika badala ya honi huku mataa yakitumia nguvu za gesi kumulika. Betri ya kwanza ilitengenezwa mwakani 1920 pale ambapo watu waliona kwamba gari lafaa liwe na nguvu nyingi zaidi za kielektroniki.

Kampuni ya Hudson ya magari ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuanza kutumia betri ya kwanza ya gari mwakani 1918 kabla haijaidhinishwa na Shirika la kukagua mabetri la Battery Council International Archived 7 Desemba 2017 at the Wayback Machine..

Uhifadhi wa betri ya gari

[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida, betri za gari huwa na mchanganyiko wa madini au electrolyte ambayo husaidia betri kuhifadhi chaji ya kielektroniki. Betri yafaa iwekwe pahali pasipo na joto jingi maana mchanganyiko huu waweza kuyeyuka (evaporate).

Vile vile, viishio vya nyaya vinavyoshikanisha betri na injini vyaweza kupata kutu au kuharibika. Kuhakikisha kwamba hili halitofanyika, wafaa uwe na mazoea ya kusafisha viishio hivi kwa grisi.

Betri haifai kuwekwa kwa muda mrefu bila chaji. Hili likifanyika, basi huenda ikaharibika. Ili kuhakikisha kwamba betri yako ya gari ina chaji kila wakati, ni vizuri kuangalia kwa kutumia kifaa kinachoitwa hydrometa (hydrometer). Unapoendesha gari kisha ukagundua kwamba haina chaji, inafaa uombe betri ya gari ya mwenzako na kutumia car jumper (lithium ion jumpstarter).

Betri inapomaliza kipindi chake cha maisha, haifai kutupwa hivi hivi kwa mabiwi. Hili ni kwa sababu huwa ina madini ya lidi ambayo ni hatari sana kwa usalama wa binadamu. Kwa kawaida, kampuni za betri huomba zile betri nzee zirudishwe kwao ili waweze kuziondoa kwa njia nzuri na salama.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.