Besifloxacin
Mandhari
Besifloxacin, inayouzwa kwa jina la chapa Besivance, ni dawa ya kukinga inayotumika kutibu mwasho wa utando wa nje wa mboni ya jicho na kope la ndani utokanao na bakteria.[1] Inatumika kama tone la jicho.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na uwekundu wa jicho.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio.[2] Usalama wake katika ujauzito hauko wazi.[2] Ni fluoroquinolone na hufanya kazi kwa kuzuia DNA topoisomerases.[2]
Besifloxacin iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya matibabu nchini Marekani mwaka wa 2009.[1] Nchini Marekani, chupa ya mililita tano inagharimu takriban dola 210 kufikia mwaka wa 2022.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "DailyMed - BESIVANCE- besifloxacin suspension". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 "Besifloxacin Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Besivance Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)