Benki ya Azania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Benki ya Azania
Makao MakuuDar-es-Salaam, Tanzania

Benki ya Azania ni benki ya biashara yenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam nchini Tanzania ambayo jina rasmi ni Adili Bancorp Limited lakini inajulikana kama Benki ya Azania.

Azania Bancorp ni taasisi ya fedha inayoweza kufanya biashara na wakulima wadogowadogo na kupata faida kubwa tu. Pamoja na Watanzania kukubali kuwa asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini na wengi wao ni wakulima na wafugaji, bado taasisi za fedha hazijafanya uamuzi wa kufanya biashara na Watanzania hao ili kupata faida hiyo.

Imesajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ambayo ndiyo Benki kuu ya Tanzania na msimamizi wa benki zote nchini.

Tarehe 19 mwezi wa 4 2018 baada ya Ushuru ilipata faida ya shilingi bilioni 1.8.[1]

Benki ya Azania ni benki ya biashara ya kiwango cha kati ambayo inatoa huduma za rejareja kwa wateja, Mikopo ya kifedha,kutoa na kubadilisha fedha za kigeni ,wanatoa barua za mkopo na ufadhili mbalimbali ndani na nchi za nje.

Azania Benki Kigezo:Mwezi wa tatu Mwaka 2017, ili kuwa inamiliki Mali yenye thamani ya dola za kimarekan Milioni 147 sawa na (TZS:332.73 billion). Inakadiriwa kuwa,kuanzia Tarehe 31 Mwezi wa Tatu 2017 hadi Mwezi watatu 2018 ,Benki ya Azania ilikuwa na hisa zenye thamani ya TSh57,880,000,000 sawa na (dola Milioni 25.6 ).[2] Kufuatia kupatikana kwa mali na madeni ya Benki M, mnamo Januari 2019, mali yote ya Benki ya Azania ilithaminiwa takriban dola za Kimarekani milioni 582 sawa na (TZS: bilioni 1,339).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Lamtey, Gadiosa (18 April 2018). Azania Bank posts Sh1.8 billion profit after tax.
  2. Azania Bank (24 April 2017). Azania Bank Limited: Financial Condition As At 31 March 2017 (PDF). Azania Bank Limited.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Benki ya Azania kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.