Nenda kwa yaliyomo

Uwanja wa Taifa (Tanzania)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa michezo wa Taifa, Tanzania
Muonekano wa juu wa Uwanja
Jina maarufuUwanja wa Benjamin Mkapa
EneoTemeke, Dar es Salaam
Ufunguzi2007
Uwezo60,000
Aina ya nyasiNyasi asilia

Uwanja wa Taifa wa Tanzania unajulikana pia kama Uwanja wa Mkapa ni uwanja wa michezo unaopatikana nchini Tanzania katika mkoa wa Dar es Salaam.

Uwanja huo, uliojengwa karibu kabisa na uwanja wa uhuru, uwanja wa zamani wa taifa wa Tanzania, ulifunguliwa rasmi mwaka 2007.

Uwanja huo unatumika pia kwa ligi kuu ya mpira wa miguu pamoja na sherehe au matukio mbalimbali ya Kitaifa na yasiyo ya Kitaifa.

Ni kati ya viwanja vikubwa vya michezo barani Afrika ukiwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 60,000 na pia ni uwanja mkubwa zaidi wa michezo nchini Tanzania, uwanja huu ulijengwa na kampuni ya wachina ya Beijing Construction Engineering Group kwa gharama za dola za kimarekani milioni 56.

Mechi ya mwanzo katika uwanja huo ilikuwa ni kati ya Simba S.C. na Young Africans S.C.[1]

Marejeo