Ben Okri
Ben Okri (alizaliwa 15 Machi 1959) ni mshairi na mwandishi wa riwaya kutoka Nigeria. Alikaa mjini London miaka yake ya utotoni, lakini alirudi Nigeria mnamo 1968. Alirudi Uingereza tena mwaka wa 1968 ambapo alijiuunga na Chuo Kikuu cha Essex. Amepokea shahada ya heshima kutoka Chuo Kikuu cha Westminister (1997)na Chuo Kikuu cha Essex (2002_ na alipwa tuzo la OBE mnamo mwaka wa 2001.
Tangu achapishe riwaya yake ya kwanza, Flowers and Shadows (1980)(Maua na Vivuli), umaarufu wa Okri umeenea Duniani kote, na mara nyingi hutazamwa kama mmoja wa waandishi wazuri zaidi wa Afrika. Kitabu chake maarufu zaidi, The Famished Road (Njia yenye njaa), kilipewa tuzo la 1991 la Booker. Ameshinda Tuzo la Waandishi wa jumuiya ya Madola, Tuzo la Agha Khan la Uandishi Bunifu na alipewa Tuzop la Crystal na Baraza la Uchumi Duniani. Pia yeye ni mwanachama wa Shirika la Kifalme la Fasihi.
Ametazamwa kama mhalisia wa miujiza, ingawa amekataa kutambulika hivyo. Uzoefu wake wa kwanza wa moja kwa moja wa vita vya wenywe kwa wenyewe nchini Nigeria unasemekana kumpa msukumo wa kuandika viotabu vyake vingi. Yeye huandika mambo ya kawaida nay a kimetafizikia, ya binifasi na ya kijamii, huku akimvuta msomaji na maelezo yake ya kina.
Okri ni makamu wa rais wa Kituo cha Kiingereza cha shirika la kimataifa la PEN, ambalo ni shirika la waandishi lenye matawi 130 katika nchi 100. Pia, yeye ni mwanachama wa Sinema ya Kitaifa ya Uingereza. Anaishi mjini Lodnon.
Baada ya kupumzika kwa miaka 5, kitabu cha kumi na moja cha Okri, , Starbook (Kitabu cha Nyota) kilichapishwa na Rider. Hadithi za Uhuru, riwaya ndogo na mkusanyiko wa hadithi fupi kilichapishwa mnamo mwaka wa 2009.
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]- 1987 Tuzo la waandishi wa Jumuiya ya Madola (Eneo la Afrika, Kitabu Kizuri Zaidi) - Incidents at the Shrine (Matukio katika Dhehebu)
- 1987 Tuzo la Aga Khan la fasihi bunifu - Incidents at the Shrine (Matukio katika Dhehebu)
- 1988 Tuzo la Guardian la Fasihi Bunifu - Stars of the New Curfew (alikuwa miongoni wa waandihsi bora zaidi)
- 1991 Tuzo la Booker kwa fasihi bunifu- The Famished Road (Barabara Yenye Njaa)
- 1993 Tuzo la Kimataifa la Uandishi la Chianti Ruffino-Antico Fattore - The Famished Road (Barabara Yenye Njaa)
- 1994 Premio Grinzane Cavour (Uitalia) -The Famished Road (Barabara Yenye Njaa)
- 1995 Tuzo la Crystal (Baraza la Kiuchumi la Dunia)
- 2000 Premio Palmi (Uitalia) - Dangerous Love (Mapenzi ya Hatari)
- 2008 Tuzo ya Kimataifa ya Uandishi ya Sada (Sherehe ya Kimataifa ya Fasihi ya Novi Sad Literature, Serbia).
Maandishi yake
[hariri | hariri chanzo]- Flowers and Shadows (Maua na Vivuli), (riwaya); Longman, 1980
- The Landscapes Within(Mandhari za Ndani) (riwaya); Longman, 1981
- Incidents at the Shrine (Matukio katika Dhehebu) (riwaya); Heinemann, 1986
- Stars of the New Curfew (short stories); Secker & Warburg, 1988
- The Famished Road (Barabara Yenye Njaa) (riwaya); Cape, 1991
- An African Elegy (Shairi la Maombolezi la Kiafrika) (shairi); Cape, 1992
- Songs of Enchantment (Nyimbo za Kushawishi)(riwaya); Cape, 1993
- Astonishing the Gods (Kuwashtua miungu) (riwaya); Phoenix House, 1995
- Birds of Heaven(Ndege wa Binguni) ; Orion, 1995
- Dangerous Love (Mapenzi Hatari) (riwaya); Phoenix House, 1996
- A Way of Being Free (Njia ya kuwa Huru) (insha); Phoenix House, 1997
- Infinite Riches (Mali yasiyoisha) (riwaya); Phoenix House, 1998
- Mental Fight (Kukimbia kwa Akili) (ushairi); Phoenix House, 1999
- In Arcadia (Katika Arcadia) (riwaya); Weidenfeld & Nicolson, 2002
- Okri, Ben (Agosti 2007). Starbook. Rider. ISBN 9781846040825.
- Okri, Ben (Aprili 2009). Tales of Freedom. Rider. ISBN 9781846041570.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Ben Okri's MySpace page
- The Ben Okri Bibliography - an extensive bibliography of works by and about Ben Okri. Also includes a short biography and an introduction to his work.
- Ben Okri Archived 28 Septemba 2006 at the Wayback Machine. - biography with short descriptions of selected works
- Audio: Ben Okri in conversation on the BBC World Service discussion programme The Forum
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ben Okri kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |