Belize City

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Belize City inavyoonekana kutoka baharini
Daraja la kufungulia bandarini

Belize City ni mji mkubwa kabisa wa Belize. Zamani ilikuwa pia mji mkuu lakini baada ya kuharibiwa na dhoruba ya tufani mwaka 1961 mji mkuu mpya uliundwa kwa jina la Belmopan.

Mji ulikua tena baada ya tufani kuwa na wakazi 50,000 hadi 60,000. Belize City ni kitovu cha uchumi na utamaduni na pia bandari kuu ya nchi kando la bahari ya Karibi.

Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Belize City kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.