Batilda Salha Burian

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Batilda Salha Burian (alizaliwa 19 Oktoba 1965) [1]) ni Mbunge katika Bunge la Tanzania. Aliingia 2005 kwa kiti cha wanawake kupitia chama cha CCM.

Alisoma shahada ya uhasibu kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akaajiriwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kama naibu katibu mkuu. Kanisa lilimruhusu kuendelea na masomo yake huko Uingereza kwenye vyuo vikuu vya Sussex na London alipoongeza astashahada ya uhasibu na PhD.

mnamo mwaka 1994 - 1997 aliajiriwa na Ofisi ya Rais akaendelea na shughuli mbalimbali serikalini.

Mwaka 2005 alipewa kiti cha wanawake bungeni akawa waziri msaidizi baadaye waziri. Tangu Februari 2008 amekuwa waziri wa mazingira katika ofisi ya Makamu wa Rais. Mnamo 2015-2016 alikuwa balozi wa Tanzania nchini Japan. [2][3]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Crystal personal.svg Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Batilda Salha Burian kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.