Basseterre

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Basseterre

Mji wa Basseterre (Saint Kitts na Nevis)
Habari za kimsingi
Utawala Shirika raia za Saint George na Saint Peter
Anwani ya kijiografia Latitudo: 17°18′N
Longitudo: 62°44′W
Kimo 15 m juu ya UB
Eneo 6.1 km²
Wakazi - mji: 15,500 (2005)
Msongamano wa watu watu 2,541 kwa km²
Simu +1869 (nchi yote)
Mahali

Basseterre ni mji mkuu wa shirikisho la Saint Kitts na Nevis ambalo ni nchi ya visiwani ya Antili Ndogo kwenye Bahari Karibi. Idadi ya wakazi ni takriban 15,500 (2005).

Mjini kuna kitovu cha kiuchumu wa visiwa, uwanja wa ndege na viwanda vya sukari.

Mwimbaji Joan Armatrading alizaliwa Basseterre kabla ya kuhamia Uingereza na wazai wake akiwa mtoto.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Basseterre iliundwa na Wafaransa 1627 ikawa mji mkuu wa koloni ya Kifaransa ya St. Christophe. 1627 pamoja na kisiwa chote ilitwaliwa na Uingereza.

Basseterre iliharibiwa kabisa mara kadhaa kutokana na vita, matetemeko ya ardhi, tufani na moto.