Atlantis, The Palm

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Atlantis ilipokuwa karibu kumalizwa ujenzi, mnamo Mei 2008

Atlantis, The Palm ni hoteli iliyomo Palm Jumeirah mjini Dubai. Hoteli hii inamilikiwa na washirika wawili: Kerzner International Limited na Istithmar PSJC. Ilifunguliwa tarehe 24 Septemba 2008. Hoteli hii inafanana na Atlantis, Paradise Island mjini Nassau, Bahamas.

Maendeleo[hariri | hariri chanzo]

Hoteli hii ina minara miwili inayounganishwa kwa daraja, pamoja na jumla ya vyumba 1539. Kuna stesheni mbili za Palm Jumeirah Monorail zinazounganisha hoteli hii na sehemu kuu ya visiwa vya Palm Jumeirah.


Tarehe 2 Septemba 2008, moto uliwaka kwenye ukumbi wa hoteli iliyokuwa karibu kumalizika kujengwa, saa 7:20 asubuhi na ikazimwa masaa matatu baadaye. Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika moto huo, iliyosemekana kuanzishwa na wafanyakazi waliokuwa wakifanya shughuli za kuchoma vyuma au kwa sababu ya tatizo la umeme. Ingawa dari la ukumbi uliharibika na upande wa nje ya hoteli uliharibika kutokana na moshi, hoteli hii ilifunguliwa tarehe iliyopangwa - 24 Septemba. [1]

Vivutio[hariri | hariri chanzo]

Hoteli hii ya nyota sabaina vivutio kama mahali pa kutizama wanyama wa baharini panapoitwa Aquaventure (iliyo na upana wa mita 160,000), ukumbi wa mkutano na 20,000 square feet (1,900 m2) nafasi ya rejareja. Hoteli hii pia ina Dolphin Bay (45,000 mita mraba) ambapo wageni wanaweza kuogelea na kucheza na samaki hawa. [2] Palm Jumeirah yenyewe ni sehemu moja kati ya tatu: Palm Jebel Ali na Palm Deira, ambazo bado zinajengwa.[onesha uthibitisho]


Hoteli hii inajulikana kwa kuhifadhi papa mdogo wa kike kwenye bwawa la maji ya lita milioni 1 [3], ingawa wanamazingira na shirika la PETA wanaomba papa huyu aachiliwe.

Uzinduzi rasmi[hariri | hariri chanzo]

Orodha ya wageni waheshimiwa ambao walihudhuria tukio hili ni [[Shahrukh Khan, Rani Mukerji, Lily Allen, Robert De Niro, Priyanka Chopra, Denzel Washington, Janet Jackson, Sara, Dugez York, Charlize Theron, Sir Richard Branson, The Jonas Brothers, Mischa Barton, Chris Tucker, Michael Jordan, Wesley Snipes, Andrea Colognoli]] na Lindsay Lohan na wengineo. Waimbaji kama Kylie Minogue kutoka Australia na Nawal Al Zoghbi, kutoka Lebanon waliimba kwenye tukio hili. Kulikuwa na mabaruti takriban 100,000, takriban mara saba zaidi ya mabaruti yaliyotumika kwenye ufunguzi wa Olimpiki ya Beijing mnamo 2008, ambayo ilidumu tu karibu dakika tano lakini gharama yake ilikuwa dola milioni 16.


Onyesho la mabaruti hadi kilometa 5 ya Palm Jumeirah, ilisemekana kuonekana kutoka angani. Vifaa vilivyotumika vilitoka nchi za kigeni.

Kwenye Runinga[hariri | hariri chanzo]

Mashindano wa mguu wa 6 wa kipindi cha The Amazing Race 15 ilifanyika katika bwawa lake la maji. Washindani wote 14 walipaswa kushuka kwenye bembea ya maji ya Leap of Faith, iliyowashusha kwenye dimwi lenye papa. Baada ya kupata kidokezo, timu zilipaswa kutafuta bahari iliyokuwa karibu, ambayo ilikuwa mahali pa mapumziko pa sita katika mbio. Hata hivyo, timu 13 pekee ndio iliyofaulu kushuka kwenye bembea, kwani timu moka ya Mika ilikuwa na hofu na uoga wa kuruka mahali parefu. Mwaka wa 2009, kipindi kimoja cha The X Factor ilirikodiwa katika hoteli, pale Dannii Minogue alipochagua mshindani yupi wa kike atamuunga katika burubani .

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: