Arsinoe II

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Arsinoe II (Kigiriki: Ἀρσινόη, takriban 316 KK - kati ya 270 na 268 KK) alikuwa malkia wa Milki ya Kiptolemaio na mshirikishi wa ufalme huo wa Misri ya Kale. Alipewa cheo cha Misri "Mfalme wa Misri wa Juu na Chini", hivyo kuwa Farao pia.

Arsinoe alikuwa Malkia wa Thrace, Anatolia, na Masedonia kupitia ndoa yake na Mfalme Lisimako. Alikuja kuwa mshirikishi wa ufalme wa Kiptolemaio baada ya ndoa yake na ndugu yake, Firauni Ptolemy II Philadelphus.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Arsinoe II kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.