Anne-Marie Goumba
Anne-Marie Goumba (amezaliwa 9 Oktoba 1954) ni mjumbe wa Bunge la Jamhuri ya Afrika ya Kati na kama mjumbe wa Bunge la Afrika na kutoka Jamuhuri ya Afrika ya Kati. Pia ni mke wa mwanasiasa wa muda mrefu wa Afrika ya Kati Abel Goumba.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Anne-Marie Mbakondo alizaliwa tarehe 9 Oktoba 1954 huko Nyanza, Rwanda. Kwanza alianza masomo ya juu katika École Normale Supérieure huko Save, Rwanda, kabla ya kuendelea kusoma Chuo Kikuu cha Catholique d'Afrique Centrale. Baadaye alichukua jukumu la kufundisha kama profesa katika Kitivo cha Tiba cha Butare kati ya nwaka 1973 na 1977. Alipokuwa huko, alikutana na Abel Goumba, ambaye pia alikuwa mhadhiri wa maswala ya afya ya umma, baadaye wakaoana.[1]
Kazi ya kisiasa
[hariri | hariri chanzo]Mumewe alikuwa mrekebishaji wa kisiasa wa Afrika ya Kati kwa muda mrefu, ambaye alianzisha kile hatimaye kilikua chama cha Patriotic Front for Progress. Yeye pia aliunga mkono kazi ya FPP, na alisimama katika uchaguzi mkuu wa Afrika ya Kati mwaka 2005 na alichaguliwa kama naibu wa wilaya ya tano ya Bangui na asilimia 37.32 katika marudio ya 8 Mei. Katika uchaguzi huo huo, mumewe alipoteza kiti chake. Baada ya kutajwa kwa Bunge la Jamhuri ya Afrika ya Kati, aliteuliwa kama mwakilishi wa Afrika ya Kati kwa Bunge la Afrika.[1] Mnamo Januari 2015, alisifu juhudi za kulinda amani nchini Rwanda, akisema kwamba wakati ameishi katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati kwa miaka 30, hasahau kamwe kwamba alitoka Rwanda.[2] Yeye ndiye mratibu wa shirika lisilo la serikali la Les Flamboyants, ambalo linataka kuzuia unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 Bradshaw, Richard; Fandos-Rius, Juan (2016-05-27). Historical Dictionary of the Central African Republic (kwa Kiingereza). Rowman & Littlefield. ISBN 978-0-8108-7992-8.
- ↑ 31 Jan, 2015 | Rw, aNews |. "Rwandais de Centrafrique : Rapatriés au vu du comportement des RDF | La Voix De La Diaspora Rwandaise" (kwa Kifaransa). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-21. Iliwekwa mnamo 2021-06-20.
{{cite web}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ http://www.journaldebangui.com/article.php?aid=9559
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Anne-Marie Goumba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |