Nenda kwa yaliyomo

Anna Tumadóttir

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'

Anna Tumadóttir
Picha imechangiwa na Sara Jordan Photography
Kazi yakeMkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la faida nchini marekani


Anna Tumadóttir ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la faida nchini Marekani, Creative Commons, tangu Aprili 2024.

Anna alilelewa katika nchi kadhaa, zikiwemo Iceland, Scotland, na Malawi. Alisoma Norway na kisha kuendelea na masomo yake Marekani na Afrika Kusini.

Alianza kazi yake kitaaluma akifanya kazi kwa makampuni ya masoko, akibobea katika eneo la uendeshaji kwa zaidi ya muongo mmoja.[1] Aliingia Creative Commons mwaka 2019 kama Mkurugenzi wa Bidhaa. Kisha mwaka 2021 alipandishwa cheo na kuwa Afisa Mkuu wa Uendeshaji.[2] Mnamo Januari 2024, Catherine Stihler, ambaye alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Creative Commons[3] wakati huo, alijiuzulu, na Tumadóttir akaanza nafasi kama kaimu Mkurugenzi Mtendaji. Tarehe 10 Aprili 2024, Bodi ya Wakurugenzi ya Creative Commons ilimteua kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa shirika hilo.[4] Anaishi Austin, Texas.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Anna Tumadóttir". Creative Commons (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-04-13.
  2. "Announcing Creative Commons' New CEO, Catherine Stihler". Creative Commons (kwa American English). 2020-07-09. Iliwekwa mnamo 2024-04-13.
  3. Legrand, Emmanuel (2024-01-02). "Creative Commons starts search for new CEO as Catherine Stihler steps down". Creative Industries News (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-04-13.
  4. Tumadóttir, Anna (2024-04-10). "Anna Tumadóttir Appointed as CEO of Creative Commons". Creative Commons (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-04-13.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Anna Tumadóttir kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.