Andy Warhol

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Andy Warhol mwaka 1977

Andy Warhol (jina la kuzaliwa ni Andrew Warhola, 6 Agosti 1928- 22 Februari 1987) alikuwa kati ya wasanii mashuhuri wa Marekani katika sehemu ya pili ya karne ya 20. Anakumbukwa kama mwanzilishaji wa mtindo wa Pop Art alioitekeleza katika picha na filamu.

Asili zake[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa Pittsburgh kwenye jimbo la Pennsylvania. Wazazi walikuwa wahamiaji kutoka Slovakia baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na baba alifanya kazi katika migodi ya makaa.

Msanii wa matangazo[hariri | hariri chanzo]

Baada ya shule Andy alisoma uchoraji kwenye Carnegie Institute of Technology mjini Pittsburgh (sasa Carnegie Mellon University). 1949 alihamia New York City akawa mchoraji kwa ajili ya magazeti na biashara ya matangazo. Tangu 1952 alianza kuonyesha michoro yake katika maonyesho. Alipata jina nzuri akaajiriwa na kampuni ya muziki RCA Records na kutunga kawa kwa sahani za santuri.

Kubuni Pop Art[hariri | hariri chanzo]

Tangu 1960 alianza kutumia teknolojia ya kuchapisha kwa kutumia sten seli ya kitambaa.

Alitumia picha zilizopatikana katika mazingira ya kila siku. Aliona wasanii wenzake mara nyingi walichora picha zisizoeleweka na watu wa kawaida. Kinyume chake aliamua kutumia picha zilizopo katika mazingira ya watu akilenga kwa "popular art" - au Pop Art. Hapa aliona sawa kutumia picha za kila siku zilizokuwa mara nyingi matangazo ya kibiashara. Alichora chupa za Coca Cola na bidhaa nyingine. Kati ya picha mashuhuri ni ile ya kopo la supu ya nyanya ya Campbell Tomato Soup.

Katika chapa zake aliendelea kutumia picha za mazingira ya kila siku kutoka matangazo au magazeti akirudia sehemu ya picha tena na tena na kubadilisha rangi. Mfano ni chapo ya Marylin Monroe.

Mwanzoni watu hawakuelewa picha zake wakidai eti hii si sanaa lakini baada ya muda watu waliongezeka waliomwelewa na kumpenda.

Warhol alianza pia kupiga filamu fupifupi.


Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Andy Warhol kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.