Andres Iniesta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Andres Iniesta

Andrés Iniesta Luján (alizaliwa Mei, 1984) ni mchezaji wa mpira wa miguu, kutoka nchini Hispania anayecheza kama kiungo wa kati kwenye klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania. Ni nahodha wa Barcelona F.C..

Iniesta alitokea La Masia,akademi ya Barcelona,baada ya kuhama mahali alipozaliwa.Alicheza kwenye klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 18 mwaka 2002.alianza kuitumikia Barcelona tangu msimu wa 2004-05 mpaka sasa.Iniesta ana mchango mkubwa Barcelona alipoiwezesha kuchukua makombe ya kihistoria miaka ya 2009 na 2015,na tuzo zake 33 zimemfanya kuwa mchezaji mwenye heshima kubwa pale Hispania muda wote.

Iniesta kuichezea Hispania ya wenye umri chini ya miaka 16,baadaye 19 na 21 kabla ya kuitumikia timu ya taifa 2006.Aliisaidia Hispania kushinda Euro 2008,akicheza kila mechi.Iniesta pia alikuwa ni mmoja wa timu ya washindi wa kombe la dunia 2010.Alifunga goli la ushindi kwenye fainali za michuano hiyo dhidi ya Uholanzi,na baada ya hapo kuwa mchezaji bora wa mechi na kuwa kwenye timu bora ya mashindano.Kwenye Euro 2012,Iniesta aliiongoza timu yake kupata ushindi wa mara ya pili mfululizo, na kuchaguliwa tena kuwa mchezaji bora wa mechi ya fainali dhidi ya Italia,na kuwa mchezaji bora wa michuano.

Iniesta anatambulika kuwa mchezaji bora kwa kipindi cha uchezaji wake na mmoja wa viungo bora wa muda wote.tangu 2009,alikuwa akichaguliwa kwenye timu bora ya UEFA kila mwaka mara sita na amekuwa akichaguliwa kwenye watu 16 bora kwenye kombe la dunia (FIFA World XI) kwenye vigezo tisa.Iniesta alishinda tuzo ya mchezaji bora wa UEFA mwaka 2012. Alikuwa mchezaji bora wa dunia wa tatu nyuma ya Messi aliyekuwa wa kwanza mwaka 2010.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Andres Iniesta kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.